25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Wabunge Uingereza waugomea mpango wa Brexit

LONDON, Uingereza

MPANGO wa Waziri Mkuu, Theresa May wa Uingereza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya (EU), umepingwa na wabunge kwa mara ya pili, huku zikiwa zimebaki siku 17 hadi muda wa taifa hili kujiondoa katika umoja huo.

Wabunge hao walipiga kura kupinga mpango wa Waziri Mkuu huyo juzi kwa kura 149, kiwango ambacho ni kidogo ikilinganishwa na kura zilizopigwa Januari mwaka huu.

Kufuatia hali hiyo, Waziri Mkuu May amesema wabunge sasa watapiga kura iwapo Uingereza iondoke katika EU bila mpango huo na iwapo hatua hiyo itashindwa  mpango mzima wa Brexit kujiondoa  uahirishwe.

Waziri Mkuu aliwasilisha ombi la dakika ya mwisho kwa wabunge waunge mkono mpango wake baada ya kupata hakikisho kisheria kuhusu msimamo wa Ireland kuhusu kujitoa katika EU.

Lakini licha ya kuwashawishi wabunge 40 wa Chama cha Conservative, haikutosha kikamilifu kubadili pigo la kura ya ushindi wa kihistoria dhidi ya mpango wake wa  Januari mwaka huu.

Katika taarifa yake baada ya kupata pigo hilo, May amesema: “Naendelea kuamini kwamba kwa kiasi kikubwa matokeo mazuri ni Uingereza kuondoka katika Umoja wa Ulaya katika namna nzuri na kwa mpango.

“Na kwamba makubaliano tuliyoyajadili ni bora na ya pekee tuliyo nayo.”

 Akifafanua mpango wake, alisema wabunge watarudi tena kupiga kura kuhusu iwapo Uingereza inastahili kuondoka EU na mpango huu au bila mpango huo.

Alisema kwamba iwapo watapiga kura kupinga mpango huo, watapiga tena kura siku inayofuata kuhusu iwapo kuidhinisha kurefushwa kwa kipengele namba 50 kinachohusu  mfumo wa sheria utakaoiondoa Uingereza katika EU kufikia Machi 29 mwaka huu.

Katika maelezo yake hayo, Waziri Mkuu May alisema kwamba wabunge itabidi waamue iwapo wanataka kuahirisha Brexit na  kuandaa kura nyingine ya maoni au iwapo wanataka kuondoka na mpango mwingine na si ulioko kwa sasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles