24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Wabunge Marekani wapiga kura kusimiamisha msaada Saudi Arabia

WASHINGTON, MAREKANI

BARAZA la Wawakilishi la Marekani linaloongozwa na Chama cha Democrat limepiga kura 248 dhidi ya 177 kuunga mkono azimio la kuacha kuiunga mkono Saudi Arabia katika mashambulio ya  jeshi inayoyaongoza nchini Yemen.

Wabunge wamesema wana wasiwasi jinsi Marekani ilivyochangia vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Yemen, ambavyo vimeua maelfu ya watu.

Wawakilishi waliopiga kura dhidi ya muswada huo wamesema kusimamisha msaada kwa Saudi Arabia kutaharibu uhusiano wa Marekani na washirika wa  kanda Mashariki ya Kati.

Wwameonya itadhoofisha juhudi zake za kukomesha usambaaji wa misimamo mikali ya  dini.

Ikulu ya Marekani imekuwa ikijitetea kuwa haina askari hata mmoja anayehusika moja kwa moja katika vita vya Yemen.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles