23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

WABUNGE MAREKANI WAITAKA KENYA IFIKIRIE UPYA UNUNUZI WA SILAHA

WASHINGTON, MAREKANI


WABUNGE watano wa Marekani wameitaka Serikali ya Kenya ifikirie upya mpango wa kununua silaha ikiwamo ndege 12 za kivita kwa gharama ya Sh bilioni 43 za Kenya.

Silaha hizo zilizolenga kutumika kupambana na wanamgambo wa Al-Shabaab wa Somalia zimeelezwa kuwa bei tajwa ni ya kifisadi na hazitoisaidia Kenya.

Wabunge wa nne wa Chama cha Republican, walioungana na wa Chama cha Democrat walisema katika barua yao kwa Balozi wa Kenya mjini hapa kuwa mkataba huo ni mbaya kwa Kenya.

Wabunge hao walimwambia Balozi Robinson Njeru Githae kuwa wao wana sababu ya kuhoji mchakato uliofikia makubaliano hayo ya ununuzi.

Aidha wabunge hao wamelitaka Bunge la Marekani kuzuia mpango huo wa mauzo na kuchunguza makubaliano yaliyolenga kuiuzia Kenya vifaa vya kijeshi ikiwamo ndege ya kufanyia mafunzo ya kijeshi na uongozi kutoka Kampuni ya  L3 Technologies ya hapa.

Walimwambia Balozi Githae kuwa L3 haina uzoefu wa kuzigeuza ndege za kilimo kuwa za kijasusi, doria na uchunguzi angani pamoja na uwezo wa kushambulia.

“Sehemu ya mchakato huu, imetutia wasiwasi. Umekaa kifisadi na Je, tafsiri kuhusu uwezo wa kampuni na vifaa ilizingatiwa kabla ya makubaliano?,” walihoji.

Kampuni nyingine tofauti zenye uzoefu mkubwa zinaweza kuipatia Kenya ndege zilizokwishajaribiwa na vifaa vyake kwa bei nafuu zaidi, “ walisema.

“Kutumia Sh bilioni 43 za Kenya kwa ajili ya ununuzi wa ndege ambazo zinaweza kupatikana kwa chini ya Sh bilioni 20 tu kutoka kampuni yenye uzoefu mkubwa hakukubaliki na uchunguzi ufanyike,” Balozi Githae aliambiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles