WABUNGE CHADEMA ‘WAMKIMBIA’ CHIZA AKIAPA BUNGENI

0
728

|Mwandishi Wetu, DodomaWabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wametoka ndani ya Ukumbi wa Bunge wakati Mbunge wa Buyungu, Christopher Chiza (CCM), akiapa.

Tukio hilo lilitokea mapema asubuhi leo wakati baadhi ya wabunge hao wakiwa  ukumbini tayari kwa kuanza kwa kikao cha bunge lakini walitoka kabla Spika Job Ndugai, hajaingia na kisha kuingia baada ya Ciza kula kiapo cha uaminifu.

Hali hiyo ilisababisha viti vya upande wanaokaa wabunge hao kuonekana vitupu huku wakonekana baadhi ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF).

Chiza ameapa leo baada ya kushinda ubunge wa Jimbo la Buyungu baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Kasuku Bilago kufariki dunia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here