WABUNGE 50 WA UINGEREZA WAJADILI KUMUONDOA MAY MADARAKANI

0
806

LONDON, UINGEREZA


KUNDI la wabunge 50 wa chama tawala cha Conservative wamekutana jana kujadili mchakato wa kumng’oa madarakani Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May.

Kundi hilo ni lile linalopinga mpango wa May kuhusu mchakato wa nchi hiyo kujiondoa kutoka Umoja wa Ulaya (EU), maarufu kama Brexit.

Hiyo ni kwa mujibu wa vyanzo vya habari vilivyonukuriwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), ambavyo havikutaka kujulikana.

Vyanzo hivyo vilisema kundi hilo la wabunge ambao ni sehemu ya kundi la wanasiasa wanaopinga uhusiano wa karibu wa Uingereza na EU ndani ya chama cha May cha Conservative walikutana juzi usiku.

Wanadaiwa walijadili wazi mustakabali wa May kama kiongozi.

Baadhi ya wabunge waliohudhuria mkutano huo wamesema tayari wamewasilisha barua za kusema hawana imani na May.

Kwa mujibu wa kanuni za chama hicho cha kihafidhina, kiongozi anaondolewa madarakani iwapo asilimia 15 ya wabunge wa chama hicho watapiga kura ya kutokuwa na imani naye.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here