28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Waandishi wa habari watakiwa kufuata maadili

Tabu-ShaibuNA ESTHER MNYIKA, DAR ES SALAAM

WADAU wa habari wamewataka waandishi wa habari kufuata maadili ya taaluma yao ili kuwezesha Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu kuwa huru na haki.

Akizungumza Dar es Salaam juzi katika Kongamano la Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam (DCPC),  Ofisa Habari kwa Umma wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu, aliyemwakilishi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, alisema wadau wote wa habari wanajua kuwa uchaguzi mara nyingi unasababisha matatizo katika baadhi ya nchi.

 

“Katika nchi yetu Mungu ametubariki hatujawahi kupata machafuko yoyote ya kivita na ninaamini ataendelea kutubariki yasitokee na hii ni kwa sababu ya undugu tuliojijengea toka enzi za waasisi wetu,” alisema Tabu.

Alisema vyombo vya habari vina jukumu la kuhakikisha linatenda majukumu yanayozingatia miiko ya taaluma, sheria na maadili.

“Ni vyema waandishi wa habari wakapata taarifa sahihi juu ya hatua mbalimbali za uchaguzi kutoka vyanzo sahihi vya uchaguzi,” alisema Tabu.

 

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Bahame Nyanduga, alisema maadili ya mwandishi wa habari ni nguzo muhimu inayojenga uwepo wa uhuru na haki.

Alisema ni wajibu wa mwandishi kuandika habari zilizozingatia maadili, ikiwemo kuthibitishwa na vyanzo husika ili ziwe na ukweli.

Alisema katika nchi nyingine zinazofuata mfumo wa demokrasia kipindi cha uchaguzi ni muhimu, kwa kuwa kinampa fursa kila mwananchi mwenye sifa kupiga kura na kumchagua kiongozi ampendaye.

Naye Mwenyekiti wa DCPC, Jane Mihanji, alisema wakati umefika sasa kwa wanahabari kuhakikisha wanazingatia maadili ili kuondoa dhana potofu iliyojengeka miongoni mwa jamii na kuichukulia taaluma hiyo kama kimbilio la wasio na ajira.

“Tunapinga vikali kutokuwa makini katika kazi yetu na ndiyo maana mwaka huu kongamano letu limekuja na mada inayosema uchaguzi huru na wa haki bila waandishi wa habari kuzingatia maadili ni ndoto,” alisema Mihanji.

 

Naye mtoa mada ambaye ni mwandishi wa habari mkongwe, Jenerali Ulimwengu, alisema hakuna asasi yoyote inayoweza kushindana na vyombo vya habari.

Alisema ni vyema waandishi wakazingatia maadili katika kipindi hiki ili uchaguzi uwe huru na haki.

Alisema ni vyema waandishi wakawa makini kuandika habari zilizo sahihi na zenye utafiti na fikra.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles