27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Waandishi wa habari waaswa kugeukia masuala ya kisayansi

Upendo Mosha, Mombasa

Nchi za Afrika Mashariki zimeshauriwa kushirikiana kwa pamoja katika kufanya tafiti mbalimbali zinazohusu athari za mabadiliko ya tabia katika Bahari ya Hindi, hatua ambayo itasaidia kupunguza hewa ukaa inayoleta adhari kwa viumbe hai.

Waandishi wa habari wa nchi hizo wamehimizwa kujikita katika kuandika habari za utafiti, mazingira pamoja na masuala ya kisayansi na kuacha kuandika habari za kisiasa ambazo zimekuwa zikileta machafuko na ukosefu wa amani katika jamii.

Mtafiti mkuu wa masuala ya bahari kutoka shirika la utafiti la (KEMFRI) nchini Kenya, James Kairo ameyasema hayo katika mkutano wa tatu wa chama cha Waandishi wa habari wa masuala ya mazingira, sayansi, afya na kilimo (MESHA) Jijini Mombasa.

Alisema kulingana hali ya mabadiliko ya tabia nchi kuendelea kuathiri viumbe hai katika bahari ya Hindi ipo haja ya serikali zote za nchi za afrika Mashariki kukutana na kushirikiana katika tafiti mbalimbali ambazo zitaleta mabadiliko na kupata ufumbuzi wa changamoto hizi.

“Nchi zote tushirikiane katika suala hiki kwa sisi wataamu wa masuala haya tukutane na tufanye tafiti zenye tija katika kudhibiti hewa ukaa ikiwa ni pamoja na kuhimiza jamii kupanda miti ya mikoko ambayo imekuwa na uwezo mkubwa wa kulinda mazingira ya baharini”alisema.

Aidha alisema baadhi ya waandishi wa habari wamekuwa wakijikita katika kuandika habari za siasa na kusahau kuandika mambo muhimu ya masuala ya mazingira Jambo ambalo limekuwa likichangia kuendelea kushamiri kwa vitendo vya uharibifu wa mazingira husasani baharini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles