WAANDAMANAJI WAHUKUMIWA VIFO MISRI

0
346

CAIRO, Misri


SERIKALI nchini Misri, imewatia hatiani watu zaidi ya 700 wa kundi la Muslim Brotherhood, ambao walishiriki maandamano yaliyosababisha kuondolewa madarakani aliyekuwa kiongozi wa nchi hii, Rais Mohammed Morsi, mwaka 2013.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC, katika hukumu hiyo ya juzi, watu 75 walihukumiwa vifo na huku wengine  47 wakihukumiwa kifungo cha maisha jela wakiwamo viongozi wa Kiislamu.

Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Amnesty International, limeiita hukumu hiyo si ya haki na imevunja katiba ya nchi hii.

Ghasia hizo ambazo zilizuka mwaka  2013 katika viwanja vya Rabaa al-Adawiya square, vilivyopo mjini hapa, mamia ya watu waliuawa na vikosi vya usalama.

Mapema mwaka huu, bunge la hapa liliwapa kinga ya kutoshtakiwa maofisa wa vyombo vya usalama waliohusika katika mauaji hayo na uhalifu ambao waliufanya kati ya Julai 2013 na Januari  2016.

BBC ilieleza kwamba, wale ambao walihukumiwa katika kesi walishtakiwa juu ya makosa yanayohusiana na usalama ikiwa ni pamoja na unyanyasaji, mauaji na kuandaa maandamano haramu.

Shirika hilo la utangazaji lilieleza kuwa  watu  75 walihukumiwa kifo tangu Julai mwaka huu na juzi adhabu hiyo ikathibitishwa na hivyo kuwa mwisho wa kesi hiyo.

Liliwataja miongoni mwa watu mashuhuri na wanasiasa kutoka Chama cha Muslim Brotherhood ambacho kilipigwa marufuku ni pamoja na kiongozi wao mkuu, Mohammed Badie, mpiga picha mashuhuri, Mahmoud Abu Zeid, maarufu kama Shawkan, ambaye amehukumiwa kifingo cha miaka mitano jela.

Mpigapicha huyo alikamatwa na kutupwa rumande, baada ya kukutwa akipiga picha za vurugu hizo za maandamano.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here