27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Vyuo saba vyasitishiwa udahili, viwili vyafungwa kwa kukosa vigezo

Asha Bani, Dar es Salaam         



Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), imesitisha masomo na udahili wa wanafunzi wapya kwa ngazi zote za masomo na katika programu kwenye baadhi ya vyuo vikuu kutokana na kukosa vigezo.

Pia imefuta vituo viwili vya vyuo vikuu na kuamuru wanafunzi wanaoendelea na masomo wahamishwe.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Jumanne Septemba 25, Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Charles Kihampa amevitaja vyuo hivyo vilivyositishiwa udahili kuwa ni pamoja na Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala nchini (KIUT), Chuo cha Teofilo Kisanji (TEKU), Chuo Kikuu kishiriki cha Marian (MARUco) na Chuo Kikuu Kishiriki cha Kumbukumbu ya Kardinali Rugambwa  (CARUMUCo).

Vingine ni Chuo cha kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU), Chuo kikuu cha Mt. Yohana cha Tanzania (SJUT-St. Marks Centers na Chuo kikuu cha Umoja wa Afrika Tanzania (UAUT), Chuo kikuu Teofilo Kisanji, Kituo cha Tabora  na Chuo kikuu Mt. Yohana cha Tanzania, Msalato (SJUT -Msalato Center).

Aidha, amevitaja vyuo vilivyositishiwa utoaji mafunzo na kuamuru wanafunzi wote wanaoendelea na masomo wahamishwe kuwa ni Mlima Meru (MMU), Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UoB), Chuo cha Eckernforde Tanga (ETU) cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta Kituo cha Arusha na Chuo Kikuu Kishiriki cha Josiah kibira (JOKUCo).

“Asitokee mwanafunzi yeyote akasajiliwa katika vyuo hivyo na wanaotakiwa kuhama wawasiliane na vyuo vyao haraka,” amesema Profesa Kihampa.

Kwa upande wake mwakilishi kutoka Bodi ya Mikopo (HELSB), Deus Changala amesema waliokuwa na mikopo wasiwe na wasiwasi itapelekwa watakapokuwa.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles