23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

VYOO BORA NI TATIZO KARATU

Na JANETH MUSHI -ARUSHA

 

SHIRIKA la Maendeleo Karatu (KDA),limetoa mafunzo  na kuhamasisha jamii wilayani Karatu kuwa na vyoo bora kila kaya kuepukana na magonjwa ya milipuko.

Mratibu wa mradi huo, Alfred Martin, akizungumza kwa na wananchi na viongozi wa vijiji vya Chemchem Kata ya Rhotia na Kijiji cha Upper Kitete kilichopo Kata ya Mbulumbulu,alisema kupitia mradi huo wanatoa elimu juu ya utunzaji wa mazingira, usafi na kuhifadhi vyanzo vya maji.

 

Alisema kuwa viongozi wa vijiji kwa kushirikiana na viongozi wa vitongoji wana wajibu wa kushirikiana na kuhakikisha wananchi wanafanya usafi katika mazingira yao ili kuepuka magonjwa ya milipuko kama vile kipindupindu.

Mratibu huyo alisema  utafiti uliofanywa kijiji cha Chemchem, asilimia 25 ya wananchi wake hawana vyoo, asilimia 20 wakiwa na vyoo bora, asilimia 30 wakiwa na vyoo vya kawaida huku asilimia 25 wakiwa na vyoo visivyo na ubora.

 

Kutokana na hali hiyo aliwataka viongozi hao kuwachukulia hatua za kisheria wananchi wanaokiuka utunzaji wa mazingira pamoja na kuchimba vyoo bora katika kaya zao.

“Sisi tutaendelea kutoa elimu na kuhamasisha jamii yote wawe na vyoo bora katika kila kaya ili kuepukana na magonjwa ya milipuko pamoja na suala zima la utunzaji wa mazingira,hivyo viongozi hakkisheni mnawachukulia hatua kali za kisheria wanaokiuka utunzaji wa mazingira na wasio na vyoo bora,”

 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Upper Kitete,Paskal Paulo,alisema katika kijiji hicho mwamko wa ujenzi wa vyoo bora umeongezeka pamoja na utunzaji wa mazingira.

 

Naye  Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Chemchem,Yasenti Amsi,alisema kuwa wanajitahidi kuhamasisha wananchi wao juu ya ujenzi wa choo bora katika kila kaya.

Alisema licha ya hali ya usafi wa mazingira kuwa chini,hali ya magonjwa ya milipuko imepungua kwa kiasi kikubwa tofauti na ilivyokuwa kipindi cha nyuma kabla hawajapatiwa elimu.

 

Baadhi  ya wananchi hao walisema kuwa suala la ujenzi

wa vyoo vya kisasa watalizingatia kwani wameshaona madhara yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles