25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Vodacom yachangisha waathirika wa tetemeko

kansa-ya-kizazi-620x308

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM

KAMPUNI ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania  imetoa namba maalumu ya kuchangia waathirika wa tetemeko la ardhi lilitokea mjini Bukoba mkoani Kagera na kusababisha vifo vya watu 16 na majeruhi kadhaa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation, Renatus Rwehikiza, aliwaomba Watanzania wote wanaotaka kuchangia waathirikahao kutuma fedha zao kwenye namba maalumu ya kupokea msaada ya kusaidia majanga mbalimbali ya 155990.

“Tukiwa kama kampuni ya mawasiliano tumeguswa na tukio hili na tunawapa pole waathirika wote na kuungana na wakazi wa Kagera kwa janga hili na tutatoa mchango wetu wa hali na mali kwa kupitia taasisi yetu ya kusaidia jamii ya Vodacom Tanzania Foundation.

“Tunawaomba Watanzania wote wenye nia ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi watume michango yao na tutahakikisha tunaifikisha sehemu inayohusika kuwasaidia wenzetu ambao wako katika mazingira magumu na wanahitaji msaada wa haraka,” alisema Rwehikiza

Alisema kupitia njia hiyo ya namba maalumu ya ”Vodacom Foundation Red Alert” 155990 ya kuchangisha fedha imewahi kurahishisha uchangishaji wa fedha kwa waathirika wa matukio yaliyotokea siku za nyuma na kuathiri wananchi moja ya matukio hayo ni milipuko ya mabomu ya Mbagala na Gongo la mboto jijini Dar es Salaam.

Kutokana na hali hiyo aliwahimiza wananchi kuitumia kama njia rahisi ya uchangiaji ambapo mwisho wa kupokea michango hiyoitakuwa Septemba 24, mwaka huu ambapo fedha hizo zitawezesha kununua vitu mbalimbali yakiwemo mahitaji kwa waathirika hao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles