23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

VLADIMIR PUTIN ASHINDA KWA KISHINDO

MOSCOW, URUSI


RAIS Vladimir Putin ameibuka mshindi kuliongoza taifa la Urusi kwa muhula mwingine wa nne wa miaka sita baada ya kujipatia ushindi mkubwa.

Ushindi huo ulitarajiwa katika upigaji kura uliomalizika juzi, ambao hata kabla ya kura zote kuhesabiwa, tayari alikuwa amejizolea asilimia 76, kwa mujibu wa tume ya uchaguzi.

Akizungumza katika mkutano uliomtangaza kushinda, Putin alisema ushindi aliopata ni matokeo ya hatua kubwa ya mafanikio aliyoyafikia katika uongozi wake.

Putin aliongeza ushindi huo ni uthibitisho wa kukubalika kwa sera zake.

Alisisitiza hana mpango wowote wa kufanya marekebisho ya katiba bali kuendeleza umoja na mshikamano.

Akijibu maswali kutoka kwa wanahabari, Putin alikwepa swali alilotakiwa kueleza kama atagombea tena katika muhula ujao.

“Kwangu kile mnachotaka kuniuliza inakuwa kama mizaha fulani hivi, hebu tuhesabu, ina maana nitasalia madarakani hadi nikiwa na miaka 100? Hapana hapana hapana,” alisema.

Ushindi huu mkubwa umekuwa na ongezeko la kura ikilinganishwa na ushindi wa asilimia 64 mwaka 2012, ambao mpinzani wa karibu wa Putin milionea Pavel Grudinin alipata asimilia 12.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles