23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Viziwi walalamikia mawasiliano usajili laini kwa alama za vidole

Derick Milton, Simiyu

Watu wenye matatizo ya kusikia (Viziwi) Mkoa wa Simiyu, wamesema wanapata tatizo la mawasiliano baina yao na watu wanaohusika katika zoezi la kusajili laini za simu kwa njia ya alama za vidole.

Wamesema tatizo hilo limesababisha viziwi wengi katika mkoa huo kushindwa kujisajili, kutokana na kushindwa kuelewana na watoa huduma wa kampuni mbalimbali ya simu wakati wa kujisajili kwa mfumo huo.

Akiongea leo wakati wa mafunzo ya siku moja kwa viziwi ambayo yameandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi Mkoa wa Simiyu, Alex Benson amesema viziwi wengi bado hawajajisajili kutokana na tatizo hilo.

“Mbali na tatizo hilo, bado viziwi wameendelea kukumbwa na tatizo la kutapeliwa na watu wenye nia mbaya kupitia simu, ambapo sasa kupitia mafunzo haya wataweza kutatuliwa changamoto hizo,” amesema.

Awali, akizungumza katika semina hiyo Meneja wa Mamlaka hiyo kanda ya Ziwa, Mhandisi Francis Mihayo amesema TCRA imeandaa mafunzo hayo kwa viziwi ili kuwajengea uelewa juu ya matumizi sahihi na salama ya mawasiliano.

“Tumekuwa tukipata malalamiko mengi kutoka kwao juu ya kutapeliwa kupitia simu, ambapo kupitia mafunzo hayo wataweza kufahamu namna bora ya kuepuka hali hiyo.

“Tunawaelimisha pia umuhimu wa kusajili laini zao kwa njia ya alama za vidole, tunatambua changamoto wanazozipata katika zoezi hili, ndiyo maana tumewaita hapa ili kuwapatia elimu na kutatua changamoto hizo,” amesema Mihayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles