Viziwi Simiyu walia na Polisi, Mahakama

0
677

 Derick Milton, Simiyu

 Watu wenye ulemavu wa kusikia (viziwi), Mkoa wa Simiyu wamelalamikia uwepo wa changamoto kubwa ya mawasiliano kati yao na idara za Jeshi la Polisi pamoja na Mahakama hali inayosababisha kukosa haki kama watu wengine.

 Hayo yamebainishwa leo Juni 13,  na Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) mkoa,  Mhandi Zephania, wakati wa kikao cha majadiliano ya kutatua changamoto hiyo na kamati za ulinzi na usalama Wilaya na Mkoa kilichofanyikia Mjini Bariadi.

Amesema kuwa changamoto hiyo ni tatizo kwao ambapo baadhi ya wamekuwa wakitumikia vifungo, kupoteza maisha kutokana na kushindwa kuelewana na watoa haki kwenye vyombo hivyo.

 “ Kuna mwenzetu mmoja yuko magereza kutokana na kesi yake kushindwa kusikilizwa kwa muda mrefu na huku hana hatia, lakini kesi haijasikilizwa kutokana na kukosekana kwa mkarimani mahakamani.

“ Kama chama tulichukua jukumu la kuiandikia barua mahakama itafute mkarimani na kumlipa kwa ajili ya kesi hiyo, lakini ilishindikana kutokana na mahakama kusema kuwa hawana pesa na hadi leo yuko gerezani kesi yake haijasikilizwa,” ameongeza Zephania.

Mwenyekiti huyo ameiomba serikali kuangalia upya mifumo ya kuajiri wafanyakazi katika taasisi hizo kuwepo kwa wakarimani ambao wataweza kuwasaidia viziwi ili nao waweze kupata haki kama watu wengine.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here