25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

VITISHO VYA TRUMP ULAYA VYAZUA WASIWASI

BERLIN, UJERUMANI


WASIWASI mkubwa umezikumba kampuni za Ulaya baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kutishia kuwa kampuni yoyote ya nje itakayoshirikiana na Iran itaadhibiwa vikali.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Heiko Maas amesema hofu ya kampuni hizo ni ya msingi, lakini akaonya kuwa itakuwa vigumu kuzilinda zile zitakazoendelea kufanya biashara nchini Iran.

Maas ameliambia gazeti la Ujerumani la ‘Bild am Sontag’ kuwa haoni njia nyepesi ya kupata suluhisho kwa ajili ya kuwalinda wafanyabiashara hao ili kuepukana na athari zitakazotokana na vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran.

Jumanne wiki iliyopita, Rais Trump aliamua kuiondoa nchi yake kwenye mkataba wa nyuklia wa Iran uliofikiwa mwaka 2015 na kutia saini amri ya kuiwekea vikwazo vipya Iran.

Licha ya Ujerumani, Ufaransa na Uingereza kuapa kwamba zitaendelea kuuenzi mkataba huo, wafanyabiashara wa Ulaya wapo njia panda kwa kuwa kampuni za nje zitakabiliwa na adhabu baada ya vikwazo hivyo vya Marekani kuanza kutekelezwa.

Maas pia amesema washirika wa Ulaya wanatafuta njia za kuhakikisha Iran itaendelea kufuata makubaliano ya mpango wa nyuklia yaliyofikiwa.

Alisema pia kuwa msimamo wa Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kuwa mpango huo unapaswa kujadiliwa kwa upana zaidi ili kushughulikia jukumu na matatizo ya Iran katika mashariki ya Kati.

Kauli ya Maas inakuja baada ya awali Waziri wa Fedha wa Ujerumani Olaf Scholz kuzungumza na mwenzake wa  Marekani, Steve Mnuchin ili kuweka uwezekano wa kuzisamehe kampuni za Ujerumani zitakazojikuta katika kundi la kuadhibiwa kwa kuendelea kufanya biashara na Iran.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles