31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

VITA VYA BIASHARA MAREKANI, CHINA VYASITISHWA

BEIJING, CHINA


VITA vya kibiashara kati ya Marekani na China ‘vimesitishwa kwa muda’ baada ya nchi hizi mbili zenye uchumi mkubwa duniani kukubaliana kuondoa vitisho vya ushuru baina yao.

Haya yanakuja wakati ambao nchi hizo zinapanga mikakati ya makubaliano mapana ya kibiashara.

Waziri wa Fedha wa Marekani, Steven Mnuchin na mshauri wa kibiashara wa Rais Donald Trump, Larry Kudlow, wamesema makubaliano hayo yaliyoafikiwa na maofisa wao na China yameweka mkakati wa kuangazia mapungufu ya kibiashara katika miaka ijayo.

Jumamosi, China na Marekani zilisema zitaendelea kuzungumza kuhusu hatua, ambazo zitaifanya China kununua bidhaa zaidi za nishati na kilimo kutoka Marekani ili kupunguza hasara ya bidhaa na huduma ya dola bilioni 335 kila mwaka baina yao.

Katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Fox nchini Marekani, Waziri Mnuchin alisema: “Tunavisitisha vita vya kibiashara. Kwahiyo, sasa tumekubaliana kusitisha vitisho vya ushuru tulivyowekeana tukiendelea kuufanyia kazi mkakati.

“Rais amekuwa wazi kabisa tangu mkutano wa kwanza na Rais Xi kule Mar-a-Lago, kwamba tutaipunguza hasara ya biashara.”

Mnuchin alisema wanatarajia kuona ongezeko kubwa la kati ya asilimia 35 hadi 45 mwaka huu pekee, la mauzo ya bidhaa za kilimo za Marekani kwa China.

Mnuchin pia ametabiri kuongezeka maradufu kwa bidhaa za nishati za Marekani katika soko la China, ambapo mauzo ya bidhaa hizo yataongezeka kwa kati ya dola bilioni 50 hadi 60 katika kipindi cha miaka mitatu hadi mitano.

Kwa muda mrefu, Rais Trump amekuwa akiilalamikia China na washirika wengine wa Marekani kuwa zinanufaika na makubaliano ya kibiashara yaliyopo kwa mgongo wa taifa lake linalopata hasara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles