Imechapishwa: Mon, Nov 13th, 2017

VITA MANENO YAIBUKA UPYA KATI YA TRUMP, KIM

WASHINGTON, MAREKANI


RAIS wa Marekani na Korea Kaskazini wameibua upya vita yao ya maneno kuhusu mgogoro wa muda mrefu wa mpango wa nyuklia wa taifa hilo la kikomunisti.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kaskazini ilimuita Trump kuwa ‘mchochezi wa vita na mzee’ na kusisitiza kuwa haiwezi kamwe kuachana na mipango yake ya nyuklia.

Rais Trump alijibu kwa kuandika katika mtandao wake wa kijamii wa Tweeter kuwa anashangaa ni kwa namna gani Kiongozi wa Korea Kaskazini anamuita yeye mzee.

Trump alisema yeye kwa upande wake, kamwe hatamuita Rais Kim Jong-un kuwa mtu ‘mfupi na mnene’.

Anasema kuwa anajaribu iko siku atakuwa rafiki wake wa karibu.

Trump awali alimkejeli kiongozi huyo mkuu wa Korea Kaskazini, kwa kumuita mwendawazimu na ‘mtu wa kuunda zana za roketi’.

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

YOUTUBE

VITA MANENO YAIBUKA UPYA KATI YA TRUMP, KIM