30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Visiwa 11 vinavyoibeba Rubondo

Kisiwa cha Mamba kilichoko katika Hifadhi ya Taifa ya Rubondo.
Kisiwa cha Mamba kilichoko katika Hifadhi ya Taifa ya Rubondo.

NA NORA DAMIAN, ALIYEKUWA GEITA

HIFADHI ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo ipo Kusini Magharibi mwa Ziwa Victoria mkoani Geita.

Mwaka 1965 kisiwa hicho kilipewa hadhi ya kuwa Pori la Akiba ambapo zoezi la kupandikiza wanyama lilianza katika maeneo yaliyoko nje ya kisiwa na mwaka 1977 ilianzishwa rasmi kuwa hifadhi.

MKuu wa Hifadhi hiyo, Massana Mwishawa, anasema ina ukubwa wa kilomita za mraba 456 ambapo kilomita za mraba 220 ni eneo lenye maji wakati kilomita 237 ni nchi kavu.

Pia anasema hifadhi hiyo ina visiwa vingine 11 ambavyo ni Izilambuba, Kalera, Rubiso, Makozi, Irumo, Mizo, Chambuzi, Chitebe, Manyila, Chitende na Nyamitundu.

“Kuna wanyama wa asili na waliopandikizwa, mnyama wa asili ni nzohe (Sitatunga) ambaye anapatikana katika hifadhi hii pekee,” anasema Mwishawa.

Moja ya visiwa vya ndege vilivyopo katika Hifadhi ya Taifa ya Rubondo ambao uhamahama na kwenda katika nchi mbalimbali duniani.
Moja ya visiwa vya ndege vilivyopo katika Hifadhi ya Taifa ya Rubondo ambao uhamahama na kwenda katika nchi mbalimbali duniani.

Anataja wanyama wengine walioko katika hifadhi hiyo kuwa ni tembo, sokwemtu, pongo, mamba, viboko, fisi maji, ngedere, kenge, ndezi, vicheche na nguchiro.

Mhifadhi huyo anasema visiwa vidogo vidogo vilivyoko katika hifadhi hiyo ni kivutio kikubwa cha utalii kwani vina mamba na ndege wanaohamahama sehemu mbalimbali duniani.

“Kama katika Kisiwa cha Irumo pale ndipo kwenye kina kirefu kwenda chini ambapo ni zaidi ya mita 70,” anasema Mwishawa.

Anasema shughuli zingine zinazofanyika ni uvuvi wa kitalii, matembezi ya masafa mafupi msituni na kwenye fukwe za ziwa, kutazama ndege na wanyama.

Naye Muikolojia Msaidizi katika hifadhi hiyo, Peter Mathew, anasema mnyama nzohe anapatikana katika hifadhi hiyo kwa sababu ina maeneo ouvu tofauti na mengine ambayo yameharibiwa na binadamu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles