26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Viongozi Taso wafukuzwa

NYAULINGO

NA SEIF TAKAZA, DODOMA

MKUTANO Mkuu Maalumu wa Chama cha Wakulima Tanzania (Taso) Kanda ya Kati umewafukuza viongozi wake wawili  waliokiuka katiba yao na kupewa siku 10 kurejesha mali walizozichukua.

Akizungumza mjini hapa juzi, Mweyekiti wa Taso Kanda ya Kati, Nyaulingo Bulamlete, aliwataja waliofukuzwa kuwa ni Katibu wa Taso Kanda ya Kati, Dk. Samson Muniko na Mweka Hazina wa Taso Kanda ya Kati, Josephine Bundala  kwa tuhuma za kwenda kinyume na katiba, taratibu na kanuni zinazowaongoza.

Alisema mkutano huo ulichukua hatua ya kuwafukuza baada ya kujiridhisha kwamba vitendo walivyofanya ni kinyume cha katiba yao.

“Tunawapa taarifa kuhusu viongozi wenzetu wawili tuliochaguliwa nao mwaka jana na ninyi mlituamini na kutupa nyadhifa hizi lakini wenzetu wametugeuka na kufanya yao kinyume na katiba ya chama chetu,” alisema Bulamlete.

Alisema viongozi hao walishindwa kutoa mikataba ya kazi kwa wafanyakazi walioko ofisini jambo linaloweza kuhatarisha heshima ya chama kwa kukiuka taratibu na sheria za utumishi.

“Pia viongozi hawa wameshindwa kuitisha vikao na mikutano ya kikatiba tangu mwaka jana  na kukipora chama uongozi mliouweka madarakani  na ninyi kwa mujibu wa Katiba na wameshindwa kulipa madeni ya wadau mbalimbali kama ilivyopitishwa katika vikao halali bila sababu za msingi. Baada ya kuona chama chetu hakiendeshwi kwa mujibu wa katiba yetu, Kamati ya Utendaji ya Kanda iliyoketi  Juni 15, mwaka huu iliamua mali zote za chama zirejeshwe katika ofisi ya Taso lakini hadi sasa bado hawajarudisha,” alisema Bulamlete.

Baada ya mkutano huo kuwafukuza, nafasi zao zimekaimiwa na makatibu wa Taso wa Singida na Dodoma ambao ni Vicent Meshack na Sombi Sombi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles