24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

VIONGOZI TARIME WAHARIBU MASHAMBA 37 YA BANGI

MKUU wa Wilaya ya Tarime, Glorius Luoga, akimkabidhi panga, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Tarime na Rorya, Andrew Satta, kwa ajili ya kuendelea na oparesheni ya kufyeka mashamba 37 ya bangi wilayani humo. Picha na Shomari Binda

NA SHOMARI BINDA,

UONGOZI wa Wilaya ya Tarime umefyeka mashamba 37 ya bangi  yenye ukubwa wa ekari 56 wilayani humo katika oparesheni ya siku mbili, imeelezwa.

Oparesheni hiyo iliongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Glorius Luoga, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Tarime/Rorya, Andrew Satta  na vikosi vya mbalimbali  ulinzi na usalama.

Vilevile, walikamata magunia 20 ya bangi kavu yenye uzito wa tani moja ambayo yalikuwa yamekwisha kuandaliwa na kutunzwa kwa ajili ya kupelekwa sokoni.

Kamanda   Satta, alisema katika oparesheni hiyo walikamatwa watuhumiwa 14 ambao wanajishughulisha na kilimo cha bangi.

Alisema watu hao  wanaendelea kuhojiwa na upelelezi utakapokamilika watafikishwa Mahakamani.

DC Luoga   akizungumzia katika Kijiji cha Nyarwana na Matongo Kata ya Kibasuka, alisema katika oparesheni zote ambazo zimekuwa zikifanyika  hiyo imefanikiwa zaidi.

Alisema kuharibiwa  mashamba na kukamatwa magunia hayo ya bangi kumetokana pia na ushirikiano kutoka kwa wananchi wa maeneo hayo.

Luoga alisema mikakati kabambe inaendelea kuandaliwa  kukomesha kilimo cha bangi ikiwamo kuanzisha kilimo cha miwa katika mabonde.

"Tulianza mapema kupambana na zao haramu la bangi na maagizo kutoka ngazi ya taifa itaendelea kutusukuma  katika mapambano haya na naamini tutafanikiwa na hizi oparesheni tunazoendelea nazo zinatusidia.

"Kuna watu ambao   wanakuwa kama wanakwamisha jitihada hiuzi sasa hatuwezi kukubaliana nao na tutawashughulikia," alisema Luoga.

Alisema muda umefika kwa wale wanaojihusisha na kilimo cha bangi kujisalimisha na kuachana na zao hilo haramu .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles