23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Vikosi vya Uturuki vyaendeleza mashambulizi Syria

WIZARA ya ulinzi nchini Uturuki imesema mashambulizi ya ardhini na angani yameendelea usiku kucha kuwalenga wanamgambo wa Kikurdi na maeneo yao nchini Syria.

Imesema vikosi vyake vinavyofanya mashambulizi ya kijeshi kaskazini mashariki mwa Syria vimekamata maeneo yaliyolengwa na kwamba operesheni hiyo iliyoanza jana inaendelea vyema.

Jana, Baraza la usalama la  Umoja wa Mataifa lilitarajiwa kukutana kuijadili Syria.

Kwenye ukurasa wake wa Twitter, wizara ya ulinzi nchini Uturuki imesema mashambulizi ya ardhini na angani yameendelea usiku kucha kuwalenga wanamgambo wa Kikurdi, kundi ambalo Uturuki inachukulia kuwa la kigaidi.

Wizara hiyo imesema ndege na magari ya kivita ya Uturuki yamefanya mashambulizi 181 mashariki mwa mto Euphrates ndani ya Syria tangu walipoanza mashambulizi juzi.

Operesheni hiyo ilianza  baada ya Marekani kuwaondoa wanajeshi wake katika eneo hilo.

Katika mpaka wa kaskazini mwa Syria, wakaazi waliingiwa na hofu na wasiwasi, wengine wakijaribu kukimbia kwa miguu na wengine kwa magari.

Katika mji wa Diyarbakir ambao wengi wa wakaazi wake ni Wakurdi kusini mashariki mwa Uturuki,wametaka kuwe na amani.

“Sababu za Uturuki kushambulia zinapaswa kuchunguzwa. Kwa nini waliingia Syria? Kwa nini mazingira yalitengenezwa hili lifanyike? Mtu anapaswa kujiuliza maswali haya. Mimi napendelea amani. hali mbaya ya amani  ni bora zaidi kuliko vita bora” alisema mkazi mmoja wa eneo hilo.

Kutokana na aibu ya jukumu la Marekani kuiachia Uturuki kufanya mashambulizi Syria, baadhi ya wakuu wa chama tawala cha rais wa Marekani Donald Trump wamemshutumu kwa kuwaacha Wakurdi wa Syria, ambao wamekuwa watiifu kwa Marekani katika vita dhidi ya kundi linalojiita Dola la Kiislamu IS.

Jumuia ya kujihami ya NATO imesema inadhamiria kuweka ‘eneo salama, ili kuwarudisha mamilioni ya wakimbizi wa Syria.

Lakini mataifa yenye nguvu kubwa ulimwenguni yanahofia hatua ya Uturuki inaweza ikazidisha machafuko na inaweza kuruhusu wafungwa wa IS kutoroka.

Rais Donald Trump ameyataja mashambulizi ya Uturuki kuwa hatua mbaya na amekana kuyaidhinisha.

Maafisa wa Kikurdi na Marekani jana walisema kuwa Wakurdi walisitisha operesheni zao zote dhidi ya kundi la IS, ili kukabili vikosi vya Uturuki vinavyoendelea kusogea ndani zaidi ya Syria.

Mustafa Bali ambaye ni msemaji wa vikosi vya Kikurdi nchini Syria (Syria Democratic Forces) SDF  amesema wapiganaji wao wamewashambulia na kuwafukuza wanajeshi wa ardhini wa Uturuki.

Uturuki imesema inalenga kuweka ‘eneo salama’ ambalo litawafukuza wanamgambo wa Kikurdi mbali na mpaka wake kisha wakimbizi milioni 2 wa Syria waweze kurudisha eneo hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles