23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Vijiji vinane vyaondokana na kero ya maji

Mohamed Hamad – Simanjiro

WANANCHI  wa vijiji 8 wilayani Simanjiro mkoani Manyara, wameondokana magonjwa ya tumbo,baada ya kupatiwa mtambo wa kusafisha maji ya bwawa, (PAULA) kutoka Serikali ya Ujerumanji kupitia asasi ya ECLAT Foundation.

Mradi huu uko Kijiji cha Sukuro kata ya Namalulu, unaonekana kuwa mkombozi mkubwa wa wananchi hao.

“Duniani miradi hii iko nane, mitambo mitano imefungwa Vetinam na kwa bara la Afrika iko mitatu, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Hospitali ya Nyamagana Mwanza na Kijiji cha Sukuro,” alisema Toima.

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Sukuro, Mwenyekiti wa asasi ya ECLAT Foundation, Peter Toima ambayo anashirikiana na Shirika la Upendo la nchini Ujerumani, alisema wananchi wa Sukuro wanajukumu la kuulinda mradi huo ili uwe endelevu.

“Tutaanza kazi ya kutengeneza technolojia zaidi na rahisi kusafisha maji ya bwawa ili yatumike vijijini tutakayoibuni wenyewe, itafanya kazi sawasawa na hii, kuchuja maji yawe safi na salama kwaajili ya wananchi wetu”alisema.

Alisema wataanza na Kijiji cha Narkauo ambako kuna bwawa linalohitaji ukarabati kidogo ili kupunguza madhara madhara ya kiafya na kiuchumi.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Sukuro, Lesawii Ropian, akizungumza na  MTANZANIA,  aliomba Serikali kuwasaidia kuondoa tope lililojaa  ndani ya bwawa.

“Bwawa hili mbali na kunufaisha wananchi wa vijiji nane vinavyozunguka Kijiji cha Sukuro, utakuwa na manufaa makubwa nchini, hivyo Serikali itusaidie katika uendelevu wake..tuendelee kunufaika nao na hata kuondokana na homa za matumbo,”alisema Ropian.

Mkazi wa Kijiji cha Lobosoit A, Leiyan Shinini aliomba maofisa idara ya maji kuwapa wananchi hamasa na umuhimu wa matumizi ya maji ili kupunguza madhara kwa wananchi.

Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Mhandisi Zephania Chaula alipongeza asasi  hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Ependo la Ujerumani kusaidia wananchi maji safi na salama.

“Tunalo tatizo kubwa Simanjiro la maji safi na salama..kama Serikali tuna mipango mingi ukiwepo mradi mkubwa wa Ruvu ambapo wananchi wataanza kunufaika nao,”alisema Chaula.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles