24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

VIJANA 10,000 WANUFAIKA NA MRADI WA UWEZESHWAJI VIJANA

|Mwandishi Wetu, Dar es Salaam



Jumla ya Vijana 10,132 kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Lindi na Mtwara wamepatiwa nyenzo na mashine za kuanzia shughuli zao mbalimbali baada ya kupatiwa mafunzo ya mradi wa Uwezeshwaji Vijana Kiuchumi(YEE).

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam wakati akipokea taarifa ya kuhitimisha mradi wa YEE uliokuwa ukitekelezwa na taasisi za Plan International, VSO, VETA na CCBRT chini ya Ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU).

“Naomba nichukue nafasi hii kuwashukuru EU kwa kushirikiana na Serikali katika masuala ya maendeleo ya vijana na kuwaomba mradi unaokuja uwafikie vijana wengi zaidi nchi nzima,” amesema.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Wakuu wa Wilaya ya Kibaha Mjini Assumpter Mshama na Kisarawe, Jokate Mwegelo ambao kwa nyakati tofauti wameulezea mradi huu kama mkombozi wa kweli wa vijana wa Kitanzania katika kujenga ujuzi na kupunguza tatizo la ukosefu ajira kwa vijana.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Uchumi wa Umoja wa Ulaya, Simon Van de Broeke amesema amefurahishwa na utekelezaji wa mradi huu ambao umebadili maisha na mitizamo ya Vijana kwenye kujiajiri na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali ya awamu ya Tano kutatua changamoto za Vijana.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk. Stephen Kebwe kwa niaba ya wakuu wa mikoa mingine, ameahidi kuwasimamia na kuwalea vijana wote wanufaika wa mradi wa YEE ili kuwawezesha kufikia malengo yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles