Vigezo vyawakosesha wanawake mikopo

0
902

Amina Omar, Tanga

Ukosefu wa vigezo vya kupata mikopo umesababisha wanawake kushindwa kunufaika na fursa ya mkopo maalumu kwa wanawake unaotolewa na Benki ya CRDB.

Hayo yamesemwa na Meneja Biashara kutoka benki hiyo Mkoa wa Tanga, Benedicta Mshanga wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonyesho ya biashara na utalii yanayoendelea jijini hapa.

Amesema benki hiyo imetoa fursa hiyo ya mikopo maalumu kwa ajili ya wanawake lakini wameshindwa kuitumia fursa hiyo.

“Wanawake wengi wameshindwa kunufaika na fursa hii ya mkopo kutokana na kukosa vigezo lakini wengine baada ya kupata mkopo biashara zimekufa,” amesema Mshanga.

Pamoja na mambo mengine, amesema lengo la benki hiyo ni kuhakikisha wanatoa kipaumbele maalumu cha kuhakikisha wanamuinua mwanamke wa Kitanzania ambapo amewashauri wanawake wajasiriamali kuhakikisha wanatumia fursa hiyo yamikopo ili kuinua mitaji yao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here