27.6 C
Dar es Salaam
Friday, November 29, 2024

Contact us: [email protected]

VIFO MAMA, MTOTO BADO TISHIO – TGNP

JOHANES RESPICHIUS-DAR ES SALAAM


MTANDAO wa Kijinsia Tanzania (TGNP), umeitaka Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kulipa kipaumbele suala la vifo vya uzazi kwa mama na mtoto ambavyo vinaonekana kuongezeka nchini.

Akizungumza katika mkutano wa wadau wa masuala ya utetezi wa wanawake Dar es Salaam jana, Mkuu wa Idara ya Utafiti na Maarifa pamoja na Uchambuzi wa Sera wa TGNP, Gloria Shechambo, alisema hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana vifo vya uzazi viliongezeka kutoka vifo 432 kati ya 100,000 hadi kufikia 550/ 100,000.

Alisema hali hii inaendelea kuwa kubwa kutokana na suala hili kutopewa kipaumbele kwenye bajeti mbalimbali zinazopitishwa, ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa mafunzo ya kutosha kuhusu afya ya uzazi salama.

“Katika mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Serikali wa mwaka mmoja, Serikali imesema kuwa inahitaji hadi kufikia 2020 vifo vya uzazi viwe vimepungua hadi kufikia vifo 250 kati ya wajawazito 100,000, jambo ambalo haliwezi kutimia kama hakutakuwa na fedha za kutosha kushughulikia suala hilo.

“Tanzania imesaini mikataba mbalimbali ukiwamo mkataba wa Abuja kwamba kutakuwa na bajeti ya afya ambayo ni asilimia 15, lakini hata hiki kidogo ambacho kimekuwa kikitengwa kimekuwa hakikutekelezwa hivyo kwa sababu sekta ya afya inamgusa kila mwananchi, ni muhimu kwa Serikali kuhakikisha fedha zinazotengwa zinapatikana na kupelekwa kwa wakati,” alisema Gloria.

Alisema kwa mwanamke kujifungua ni sehemu ya mwisho hivyo kabla hajafikia hatua hiyo, kuna mambo mengi yanayomkabili kama vile lishe, miundombinu pamoja na ukatili wa kijinsia ambayo yote yanapaswa kufanyiwa kazi na yawe salama kwake ili kumwezesha kupata uzazi ulio salama.

Alisema elimu hiyo inapaswa kwenda sambamba na uwekwaji wa fedha katika suala zima la afya ya mama na mtoto na kwamba suala hili si la Wizara ya Afya pekee bali linaunganisha sekta nyingine ambazo zinatakiwa kushiriki kwa ukaribu kama sekta ya maji, umeme pamoja na miundombinu na nyinginezo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles