23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Vifo kutokana na virusi vya corona vyafikia 60,000

Washington, Marekani

RAIS wa Marekani, Donald Trump amewaonya Wamarekani kujitayarisha  kwa  idadi ya kutisha  ya  vifo vinavyotokana  na  virusi  vya  corona katika  siku  zijazo wakati  idadi  jumla ya vifo duniani kote ikifikia 60,000.

Kesi zilizothibitishwa  na  wagonjwa wa  virusi  vya  Covid-19 nchini Marekani juzi Jumamosi imepindukia  watu 300,000, lakini Ulaya inaendelea kuadhibiwa na janga hilo ambalo limesababisha karibu nusu ya watu wote duniani kote kujifungia ndani ya majumba yao kwa  gharama kubwa ya uchumi wa dunia.

Zaidi ya vifo vya watu 45,000 duniani kote vimetokea katika mataifa  ya Ulaya, ambapo Uingereza imeripoti kiwango cha juu kipya cha vifo kwa siku, na kufikisha idadi jumla ya vifo  kuwa 4,300 kutoka  jumla ya kesi za maambukizi 42,000.

Malkia Elizabeth II alitoa hotuba maalum ya binafsi jana Jumapili kuwataka  watu  kusimama na kupambana na changamoto hii inayotokana na virusi vya corona, na  binafsi  kuwashuruku wafanyakazi wanaowahudumia wagonjwa wa Covid-19.

“Nina matumaini katika miaka inayokuja kila mmoja ataweza kujivunia ni kwa njia gani aliweza kupambana na changamoto hii,” alisema katika  hotuba  yake hiyo jana. 

Hivi sasa kuna zaidi ya kesi milioni 1.2 zilizothibitishwa za mambukizi ya virusi vya corona  duniani kote na zaidi ya watu 65,000 wamefariki tangu virusi hivyo vilipozuka nchini China  mwishoni mwa mwaka jana, kwa mujibu wa idadi iliyojumlishwa na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins.

Hata hivyo, Trump amesema Marekani inaingia katika “wakati ambao ni wa hali ya kutisha” kwa  “idadi mbaya kabisa.”

“Hii  huenda  itakuwa  wiki  ngumu  kabisa, kutakuwa  na  vifo  vingi sana,” alisema katika  Ikulu ya White House.

Wakati huo huo, Rais huyo amesisitiza kuwa Marekani haiwezi kuendelea kufungwa kwa milele.

“Mapambano dhidi ya virusi ni muhimu, lakini hatuwezi kuiharibu  nchi yetu. Nilisema tangu  mwanzo, tiba haiwezi kuwa mbaya kuliko matatizo,” alisema. 

Kitisho cha  mikusanyiko mikubwa kimeonekana tena  mwishoni  mwa  juma, mara  hii nchini  Pakistan ambako maofisa  wanajaribu kuwafuatilia na kuwaweka katika karantini mamia kwa  maelfu waumini ambao walihudhuria tukio kubwa la Kiislamu mwezi uliopita.

Zaidi ya watu 150 ambao wamehudhuria wamethibitishwa kuambukizwa na virusi vya corona hadi sasa, na watu wawili wamekufa. Wageni kutoka nchi kadhaa pia walikwenda katika tukio  hilo, ambalo lilifanyika licha ya Serikali kuomba kufutwa kutokana na kitisho cha virusi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles