Video ya Snura ‘Chura’ yafunguliwa rasmi

0
625

dsc_0026

Video ya wimbo wa Chura wa msanii Snura Mushi imefunguliwa rasmi baada ya kurudiwa kama ilivyoelekezwa na Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo.

Video hiyo ilifungiwa miezi sita tangu Mei 3 mwaka huu kutokana na madai kwamba ilikiuka maadili ya mtanzania kwa kuchezesha watu wakiwa nusu uchi.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Casmil Ndambalilo, amesema wameridhishwa na mabadiliko yaliyofanywa na msanii huyo katika video yake mpya ya Chura hivyo imefunguliwa kuanzia jana ili ichezwe kwenye vyombo vya habari.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here