VANESSA: IN LOVE & MONEY IMENIWEKA KARIBU NA MASHABIKI

0
245

Na JENNIFER ULLEMBO-DAR ES SALAAM


MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Vanessa Mdee ‘V money’, amesema ziara yake ya ‘In Love & Money’ inampa nafasi ya kukutana na mashabiki wake kwa ukaribu zaidi.

Akizungumza jijini hivi karibuni, msanii huyo alisema mara nyingi alikuwa ‘bize’ na shoo za nje, jambo ambalo lilikuwa likimnyima nafasi ya kuwapa burudani mara kwa mara Watanzania.

Alisema anaamini ziara hiyo ambayo imekuwa ikifanyika katika mikoa mbalimbali hapa nchini, itaweza kumuongezea idadi ya mashabiki.

“Unajua mara nying nimekuwa nikifanya shoo za nje ya nchi, hivyo kufanya ziara hii nyumbani ni jambo la faraja sana,” alisema V Money.

Mwanadada huyo alisema mara baada ya kukamilisha ziara hiyo, ataweza kubuni kitu kingine kitakachoweza kumuweka karibu na mashabiki wanaopenda muziki wake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here