27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Uwanja wa ndege Arusha kuboreshwa

Na Mwandishi Wetu

BARABARA ya kutua na kuruka ndege ya Kiwanja cha Ndege cha Arusha itaongezwa urefu, ili iweze kuruhusu ndege kubwa za abiria kuanzia 70 ziweze kutua na kuruka bila tatizo, imeelezwa.

Meneja wa kiwanja hicho, Elipid Tesha, alisema barabara ya kutua na kuruka ndege itaongezwa urefu kwa meta 200 na kufikia meta 1,800 kutoka 1,600 za sasa 1,800.

Tesha alisema kwa sasa kazi inayoendelea ni ujenzi wa eneo la maegesho ya ndege, ambayo yakikamilika yatapunguza msongamano kwa asilimia 30.

Alisema  shughuli nyingine ni ujenzi wa barabara ya kupita ndege kwenda katika maegesho,  ujenzi wa maegesho ya magari 350 kwa kiwango cha lami.

Pia alisema ujenzi huo wa maboresho ya kiwanja cha hicho utahusisha ujenzi wa eneo la kupumzika abiria, ofisi za waegesha ndege, kibanda cha ulinzi na vyoo.

Hivi karibuni Mbunge wa Kigoma Kusini, Husna Malima, alihoji mpango wa Serikali katika kuboresha kiwanja cha ndege cha Arusha ili wananchi wa mikoa ya Singida, Manyara, Simiyu, Manyara, Mara na Dodoma wahamasike kutumia usafiri wa ndege.

Alisema mafaniko ya uwepo wa ndege za abiria nchini ni pamoja na kutumika na wananchi. 

Akijibu swali hilo bungeni, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Issac Kamwelwe, alisema kurefushwa kwa uwanja huoko kutafanikisha ndege aina ya Bombardier ambayo inabeba abiria kuanzia 70 kutua na kuruka bila tatizo.

Kamwelwe alisema tayari bajeti imetengwa kwa ajili ya kazi hiyo, ambapo kiwanja hicho ni cha tatu nchini kwa kutua na kuruka ndege nyingi.

“Tumeweka bajeti kuendeleza kiwanja cha ndege cha Arusha na tayari tenda imetangazwa, kiwanja hiki kinaongoza kwa kutua ndege nyingi zaidi kwa siku ni biashara kubwa na ndio maana tunataka ndege ya Bombardier itue hapo,” alisema Kamwelwe.

Alisema mikoa jirani ya Arusha ya Manyara, Singida, Dodoma, Simiyu na Mara itafaidika na maboresho ya kiwanja hicho kwa kuwa wataweza kukitumia ipasavyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles