28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

UVCCM yaeleza Dk. Shein alivyokataa kuburuzwa

hamduNa Mwandishi Wetu, Zanzibar

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi  (UVCCM)  umesema wapambe na vigogo waliompigia debe na kumnadi Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein   kuwania urais mwaka 2010,  hivi sasa wamemgeuka na hata baadhi yao kumuona kikwazo.

Kwa mujibu wa Umoja huo,  vigogo hao sasa wamemgeuka na baadhi yao wanamuona kikwazo kwa msimamo wake wa mapinduzi na kuonekana mtu  asiyeyumbishwa kwa kukataa vitisho.

Kauli hiyo ilitolewa   mjini Unguja jana na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka, alipozungumza na makundi ya vijana wa CCM kutoka majimboni  ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya marudio ya uchaguzi wa Zanzibar.

Alisema madalali hao wa siasa hawakujua kama Dk. Shein ni zao la mapinduzi huku wazazi wake wakiwa ni waathirika wa Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12 mwaka 1964.

“Laiti kama Dk. Shein asingelelewa, kuandaliwa na kukuzwa kwa  misingi ya mapinduzi, mbayuwayu na mbweha wanaopania  kuyatokomeza mapinduzi yetu wangepata mwanya wa kuukwapua urithi huo.

“Waafrika wenyeji wangerudi katika kutumikishwa kazi za uyaya na ukuli na kulipwa ujira mdogo tofauti na jasho wanalolitoa,” alisema Shaka.

Aliwataka Wazanzibari kuendelea kumuunga mkono Dk. Shein wakiamini kiongozi huyo si wakala wala dalali.

“Naona fahari kukitumikia chama changu nikiwa bado kijana, nakomazwa, kufunzwa na kuelimishwa   kujua pumba na mchele. Wanaojifanya vinara wa uongo nawasikitikia kwa sababu watamalizika kwa aibu katika siasa,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles