30.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

UVCCM Lindi yampa tano Magufuli uamuzi wa serikali kununua korosho

Hadija Omary




Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa  Lindi, wamempongeza Rais John Magufuli kwa kwa uamuzi wa kununua korosho kwa bei inayomletea tija mkulima.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake wilayani Nachingwea Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Lindi, Majid Lupanda, amesema hatua iliyochukuliwa na Rais ni hatua ya kishujaa sana na imeonyesha wazi kuwa ni moja ya mfulululizo wa matendo ya kishujaa yanayofanywa  na Rais kwa masla mapana ya taifa na si maslahi binafsi

“Rais ameonyesha ushujaa mkubwa katika hili, tunampongeza sana kwa hatua nzuri aliyoichukua ya kununua korosho kwa bei yenye tija kwa mkulima, na tunamuomba Mungu azidi kumpa nguvu ya kuendelea kuitumikia Tanzania kwa maslahi mapana ya Taifa,” amesema Lupanda.

Jana, Rais John Magufuli alitangaza kusitisha ununuzi wa korosho kwa wafanyabiashara ambapo serikali imezinunua korosho hizo zote kwa bei ya kuanzia Sh 3,002 hadi 3,016 kuanzia leo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles