31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

UVCCM Iringa yamtikisa Msigwa uchaguzi 2020

NA RAYMOND MINJA, IRINGA

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Iringa mjini, Silvastory Ngerera amesema kuwa chama chao hakina mpango wa kuandaa mgombea mwenye nguvu ya kupambana na Mbunge wa Iringa mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
Mchungaji Peter Msigwa bali kimeandaa mgombea ambaye atayetatua
kero na shida za wananchi kwa kuziishi.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa na diwani wa kata ya Kitanzini, Mahadhi Hepautwa amesema lengo la chama hicho ni utekelezaji wa kazi zilizofanywa na madiwani hao tangu walipochaguliwa.

“Nimesikia mtu mmoja akisema kuwa CCM haina mgombea wa kupambana naye, mwambieni Msigwa kuwa CCM haiandai mgombea wa kupambana naye CCM inaandaa mgombea bora wa kupambana na kero na changamoto za wananchi wa jimbo la Iringa Mjini mgombea ambaye atazijua shida za wananchi wa jimbo la Iringa Mjini, ataziishi na zitamchoma kisha atachukua hatua ya kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu,” amesema Ngerera.

Aidha Mwenyekiti huyo ameeleza kuwa CCM ni chama kikubwa na kina hazina ya wagombea wa kutosha na wanachosubiri ni kusikia wananchi wa jimbo la Iringa wanataka mtu wa aina gani kwa kuwa chama hicho kina watu wenye sifa zote za kugombea na kuchukua jimbo asubuhi na mapema.

‘’Msigwa anasema anapata siri nyingi za chama chetu, mwambieni kuwa hizo anazopata ni taarifa sio siri, ila leo hii nataka nimpe siri kubwa ambayo hajawahi kuipata, siri hiyo ni kuwa kwa mwaka 2020 CCM Iringa Mjini tumejipanga kwa udi na uvumba Msigwa ni lazima atoke mjini hapa”

Ngerera amesema pia ameshuhudia madiwani wote wakielezea ni nini
wamefanya, wanafanya na wanatarajia kufanya na yote wameyafanya mbele ya viongozi wao wa chama hivyo inathibitisha kuwa CCM ni chama imara na madhubuti kinachofanya vyema kazi yake ya kuwasimamia viongozi wote waliowapa dhamana na kuhakikisha kuwa wanatekeleza ahadi zao zote kwa wananchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles