30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

UTUMWA HUKO LIBYA NA AFRIKA

Na CHARLES KAYOKA


KATIKA siku za hivi karibuni kumekuwa na kuonyeshana picha na taarifa kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na biashara ya kuuawa watumwa wa Waafrika weusi, wengi wao kutoka nchi za Afrika Magharibi, unaofanywa huko Libya. Na Tunaambiwa Rais wa Chad anasema atapeleka majeshi kuwaokoa watumwa hao na kuwaadhibu mabwana utumwa hao. Mimi nina maswali mawili makubwa ambayo nitayajibu kwa ufupi sana katika makala hii.

Kwanza kwani wanaouza watumwa na wanaouzwa utumwani wana tofauti gani ya hali? Umaskini ndio uliowapeleka Waafrika weusi na wengine huko Libya na hii si mara ya kwanza. Kuna mitumbwi na mitumbwi ya Waafrika iliopinduka Bahari ya Mediterranean na wengine kuolewa na mfereji huu wa wahamaji uliendelea kutiririka kwa miongo kama mmoja na nusu sasa huku viongozi wa Afrika wakionyesha kutojali. Baada ya kuuharibu uchumi wa Libya kwa imani kuwa Ghadafi akishatoka kutakuwa na Libya mpya, Libya mpya kwa kweli, basi uchumi utakuwa.

Kumbe umeleta umaskini. Wakimbizi wa uchumi wamekutana na maskini wenzao wenye bunduki, wakimbizi wakitafuta maisha na wenye bunduki maskini wanatafuta maisha. Mwenye nguvu anamtia utumwani asiye na Nguvu. Ni uchumi na sio roho mbaya. Mbona wakati wa Ghadafi hii haikutokea.

Lakini swali langu la pili ni kuhusiana na sakata hilo ni kukosekana kwa mkakati wa kufikiria kwa undani suala lenyewe na kuliona kama ni jambo linalojitenga. Tanzania, kwa mfano ina vijana wangapi ambao wako jela sehemu mbalimbali za dunia kutokana na kujiiingiza kwenye biashara haramu za dawa za kulevya. Hivi karibuni tumesikia vijana watatu wa Kitanzania wamekamatwa huko Swaziland wakijaribu kuingiza dawa za kulevya huko Afrika Kusini na kuna Watanzania, Wakenya na kadhalika wako huko Afrika Kusini wakiwa wahamiaji haramu. Na kuna wanaokufa wakiwa safarini kusafirisha dawa za kulevya.  Na Yule aliyefarika akiwa safarini akiwa na kete za dawa za kulevya.

Niliwahi kuombwa ushauri na dada mmoja kuhusu nini afanye kwani aliahidiwa Sh. milioni tano, za Tanzania, kama ataweza kusafirisha dawa za kulevya kwenda Afrika Kusini. Milioni mbili na nusu kabla ya safari na zinazobaki baada ya kusafirisha salama. Alisita,  tukashauriana, hakwenda, lakini kuna vijana wenzake wengi walikwenda, kama sio bado wanakwenda. Hao ni watumwa wa watu fulani ambao wanawanyonya kiuchumi, ni watu wa kufa tu. Wakikamatwa wakafungwa, wakifa kutokana na majanga mengine.

Hawa wanatofautiana na wale watumwa wa Libya. Hawa wanabahatisha maisha na wanaweza kufa na wale wanabahatisha safari na wanaweza kufa. Na kuna wengi wanakufa. Viongozi wa Waafrika wanataka kuwasingizia mabwana utumwa Libya au wauza dawa za kulevya badala ya kujichunguza na kuona kama ni wao au kuna sababu nyingine zinazosukuma kuwa na wimbi la watu wanaingizwa utumwani huko Libya au utumwa wa dawa za kulevya kwa kusafirisha, kuuza au kwa kuzitumia kama mateja. Sababu ni moja, utumwa unasababishwa na umaskini na kujiingiza katika dawa za kulevya kunasababishwa na umaskini na watu pekee wanaoweza kulitatua tatizo hili ni viongozi wa Afrika.

Uchumi unasemekana unakua, wanasema kila siku, kila baada ya uchaguzi na hata kabla, kuwa uchumi unakua, kuwa wataongeza nafasi za ajira, lakini watu maskini wanaongezeka kila siku na idadi ya watu wasioweza kupata kazi na hivyo kuamua kuhama au kujiingiza katika shughuli haramu inaongezeka. Lakini yakitokea kama yanayotokea huko Libya, tunawalaumu wale Waarabu, tunasahau sisi viongozi ndio tumesababisha kwa sababu ya kuwa na sera za uchumi zisizo na tija. Na tunasahau kuwa tuna makundi mengi ambayo hayana uhakika wa kesho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles