24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

UTAFITI: WAFANYAKAZI WENGI HAWAZIJUI HAKI ZAO

|Leonard Mang’oha, Dar es Salaam



Imeelezwa kuwa asilimia 13 ya wafanyakzi pekee ndiyo wanafahamu haki zao mahala pa kazi.

Aidha, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), umeonesha kuwa wafanyakazi wengi hawalipwi malipo ya likizo huku baadhi ya waajiri wakiwalazimisha wafanyakazi kuuza likizo zao ili walipwe malipo hayo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti ya Utafiti wa Haki za Binadamu na Biashara huo leo Alhamisi Agosti 16, jijini Dar es Salaam Ofisa Msaidizi Kitengo cha Haki za Binadamu na Biashara, Tito Magoti, amesema hali hiyo inaonesha jinsi gani wafanyakazi wengi hawaelewi haki zao.

Magoti amesema tatizo hilo limeonekana kuwa kubwa zaidi katika mikoa ya Morogoro na Mwanza na kwamba utafiti huo umeonesha kuwa no asilimia 13 pekee ndiyo wanaofahamu haki zao mahala pa kazi.

“Utafiti huu pia umebaini kuwa wafanyakazi wengi hawapati nafasi ya kujumuika ikiwamo kujiunga na vyama mbalimbali vya wafanyakazi.

“Wafanyakazi wengi hawana imani na vyama vya wafanyakazi kutokana na kwamba wapo kwa hisia za rushwa kati wa viongozi wa na waajiri,” amesema Magoti.

Ameongeza kuwa watu wengi hawajui kama kuna mafunzo yanayohusu usalama mahali pa kazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles