24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Utafiti: Uvutaji sigara husababisha upofu

LOS ANGELES, MAREKANI

LICHA ya kuwa ni mtindo uliotamalaki, hasa kwa vijana, ukweli ni kwamba uvutaji wa sigara huharibu uwezo wa kuona, kwa mujibu wa utafiti wa Chuo Kikuu cha Rutgers, New Jersey, Marekani.

Utafiti huo unatambua kuwa umri mkubwa ni moja kati ya sababu ya uoni hafifu lakini unasisitiza kwamba hata kijana anayevuta sigara hupata tatizo hilo.

Watu 134 wenye umri kati ya miaka 25 hadi 45 walihusishwa katika utafiti huo, ambapo 71 walikuwa wakivuta chini ya 15 kwa siku, huku 63 wakisema ni 20 au zaidi.

Baada ya maswali yaliyokuwa yakilenga namna wanavyoweza kuzitambua rangi mbalimbali, wale waliokiri kuvuta sigara 20 au zaidi kwa siku, walionekana kushindwa zoezi hilo, kwamba walikuwa na tatizo la uoni hafifu.

Wakifafanua namna tatizo hilo linavyosababishwa, watafiti wanasema madhara hayo yanatokana na kemikali zinazopatikana katika sigara, ikiwamo nicotine, ambazo moja kwa moja hushambulia mishipa ya damu seli za macho.

Pia, wanazitaja carbon disulphide na styrene kuwa ni kemikali zingine zinatokana na moshi wa sigara na kusababisha tatizo.

Aidha, wataalamu wa afya wanadai kuwa hata magonjwa kama kisukari au majeraha katika eneo la ndani ya jicho liitwalo retina ni sehemu ya sababu za uoni hafifu, hasa tatizo la kutambua na kuweza kuzitofautisha rangi, changamoto kubwa ikiwa ni kutofautisha nyekundu, njano na kijani.

Katika maelezo yake juu ya utafiti wao uliochapishwa katika jarida la journal Psychiatry Research, ambaye ni Mkurugenzi wa Tafiti za Chuo Kikuu cha Rutgers, Dk. Steven Silverstein, anasema:

“Uvutaji wa sigara una madhara makubwa kiafya,” anasema na kuongeza huathiri sehemu ya ubongo inayohusika na matendo ya hiari, uwezo wa kufikiri na hupunguza utendaji kazi wa eneo la ubongo linaloshughulikia uwezo wa kuona.”

Tatizo linaonekana kuwa kubwa Marekani kwani takwimu zinaonesha kuwa watu milioni 34.3 wameifanya sigara kuwa ni starehe yao. Wakati zaidi ya milioni 16 wakisumbuliwa na magonjwa yatokanayo na bidhaa hiyo, 12 wanalalamikia matatizo ya macho.

Ni tofauti kidogo na Uingereza, ambako uvutaji sigara umepungua kwa asilimia 17.2 kwa takwimu za tangu mwaka 2015.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles