27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Usiyoyajua kuhusu komamanga

Komamanga
Komamanga

KOMAMANGA ni tunda lenye asili ya India na Persia, kwa jina la kisayansi linaitwa Punica Granatum. Lakini lililetwa Marekani na wawekezaji wa Kihispania na kwa sasa limejulikana dunia nzima. Komamanga si tunda tu, bali ni chakula chenye vitamini, madini pamoja na virutubisho vingine vingi vinavyoweza kufanya miili yetu kuwa na afya na nguvu tele. Virutubisho vinavyopatikana katika komamanga ni vitamin C kwa wingi, vitamin B5, vitamin A, vitamin E, Madini ya Potassium na Iron.

Juisi ya mbegu za komamanga husaidia kuponya saratani, pia husaidia mtiririko wa damu kwenda vizuri katika mishipa ya damu, hivyo kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo, shinikizo la damu na kiharusi.

Huzuia meno kuoza na kuhuisha mfumo wa kinga mwilini kwa kuondoa vijidudu, bakteria na maambukizi ya virusi ndani ya mwili.

Pia husaidia kutibu maradhi ya tumbo ikiwamo kutopata choo. Komamanga hutumika kama tunda, kutengeneza juisi, pia hutumika likiwa limepikwa.
Mti wake una faida nyingi mno  katika mwili wa mwanadamu.

Una virutubisho vingi  vinavyopatikana kwenye  magome, majani, mbegu, maganda ya matunda, juisi  ya  matunda pamoja  na kwenye  maua  ya  mti wake.

Zifuatazo  ni  faida  muhimu  za  mti  wa  mkomamanga:

1. Maganda ya tunda la mkomamanga yakichemshwa hutoa juisi ambayo hutumika  kama dawa ya kufunga kuhara.

2. Majani ya mkomamanga hutumika kutibu hali  ya  tumbo  kujaa  gesi na kudhibiti tindikali  (acid) tumboni.

3. Majani ya mkomangana hutumika pia katika kutibu tatizo la kuhara  damu maambukizi ya bakteria katika kibofu cha mkojo.

4. Rojo ya mbegu za mkomamanga ikichanganywa na maziwa ya ng’ombe, hutumika kutibu tatizo la mawe kwenye figo.

5. Fukuto ya komamanga husaidia kutibu minyoo aina ya tegu pamoja na uvimbe wa wengu.

6. Komamanga husaidia katika kutibu tatizo la vidonda vya  tumbo.

7. Komamanga pia ni mahiri  katika kutibu magonjwa ya  kusendeka (magonjwa ya muda  mrefu), kama vile saratani ya tezi  dume, saratani mbalimbali, kisukari, baridi yabisi na uvimbe  katika maungio ya vidole (gout)

8. Komamanga husaidia kuondoa sumu mwilini.

9. Husaidia katika kupambana na tatizo la uzito mwilini.

10. Husaidia kuua virusi vya aina  mbalimbali mwilini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles