Imechapishwa: Sat, Oct 7th, 2017

USHAHIDI MPYA AJALI YA NDEGE MALAYSIA WATOLEWA

DONETSK, Ukraine

WACHUNGUZI wa kujitegemea kutoka  Jamhuri ya Watu wa Donetsk (DPR),  wametangaza kuwa wamepata ushahidi mpya unaothibitisha kuwa  kombora aina ya  Buk ndilo lililotumika kushambulia  ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia ambayo ilianguka  Mashariki mwa Ukraine mwaka 2014.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Donetsk (DAN), taarifa hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa Idara ya Uchunguzi kutoka  Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Jamhuri  hiyo, Roma Belous.

DAN ilisema kutokana na ushahidi huo mpya kuhusu  ajali hiyo iliyotokea nje kidogo mwa Jimbo la  Torez, Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu nchini humo imefungua kuhusu kosa hilo la  jinai.

Alisema wachunguzi wana taarifa mpya zinazothibitisha kuwa kombora hilo lilirushwa  kwa mfumo wa kombora hilo aina ya Buk kutoka eneo la  makazi lililopo katika mji wa  Zaroshchinskoye uliopo katika Wilaya ya Shakhtersky, ambalo lilikuwa linadhibitiwa na Jeshi la Ukraine wakati ajali hiyo ilipotokea.

Akizungumza  kuhusu uchunguzi huo, mpatanishi mkuu kutoka Jamhuri hiyo ya Donetsk,  Denis Pushilin, alisema nchi yake  ilikuwa na hamu ya kupata uchunguzi tofauti na uliopatikana awali kuhusu ajali hiyo.

“Tuna matumaini kuwa licha ya shinikizo la kisiasa, uchunguzi  huu wa kimataifa utaonesha kutokuwa  na ubaguzi na mtazamo chanya  katika kuchunguza ajali na kupata chanzo cha ukweli kuhusu waliohusika kusababisha msiba ambao uligharimu  maisha ya raia wasio na hatia,” alisema Pushilin.

Ndege hiyo aina ya  Boeing-777  mali ya Shirika la Ndege la  Malaysia, ilianguka  Julai 2014 wakati ikiwa njiani kutoka katika mji mkuu wa Uholanzi, Amsterdam kwenda katika mji mkuu wa Malaysia wa Kuala Lumpur na kusababisha vifo vya watu  298 wengi wao wakiwa ni raia wa Uholanzi.

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

YOUTUBE

USHAHIDI MPYA AJALI YA NDEGE MALAYSIA WATOLEWA