33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

USAJILI 2017/2018 UWE WA MALENGO

USAJILI wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2017/2018 ulifunguliwa rasmi na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) mwishoni mwa wiki iliyopita,  ukitarajiwa kufika tamati Agosti 6 mwaka huu.

Baadhi ya timu zinazotarajiwa kuonekana msimu ujao wa Ligi Kuu zilianza kufanya usajili kwa kuhakikisha zinatimiza malengo ya kupata vikosi vilivyo na ubora.

Kwa ujumla, michuano ya msimu uliopita  iliweza kuonyesha ushindani  licha ya baadhi ya timu   kuonekana kuwa wasindikizaji hali iliyosababishwa  zishindwe  kufanya vizuri kutokana na usajili mbovu.

Matarajio ya watanzania na mashibiki wengi wa soka kwa sasa ni kuona timu zao zikifanya usajili wa kueleweka na siyo bora usajili kwa sababu    mara nyingi imeshuhudiwa usajili  usio na tija ukiwagharimu viongozi  msimu unapoanza na kusababisha   wachezaji kushindwa kuonyesha viwango vyao kwa kuishia kukaa benchi.

Hadi sasa klabu za Simba, Yanga, Azam FC na Singida United zimeweza  kutimiza nusu ya idadi ya wachezaji wanaotakiwa kusajiliwa huku zikitumia muda huu wa usajili kumalizia baadhi ya sehemu zilizoonyesha upungufu.

MTANZANIA tumezoea kushuhudia Simba, Yanga na Azam zikiendelea kuwa juu kwa kuhakikisha zinajipanga kusajili wachezaji bora ingawa wakati mwingine usajili huo umekuwa ukishindwa kuziwezesha timu hizo kufikia malengo na azma zinayowekea kwa msimu husika.

Timu hizo kuendelea kuwa tishio katika usajili ni ishara nzuri. Zinapaswa kupongezwa kwa hatua zilizoweza  kufikia kwa sababu licha ya dirisha kufunguliwa rasmi, tayari zilikuwa zimeweza  kunasa saini za wachezaji mbalimbali.

Hiyo inaonyesha kwamba timu nyingine zimekuwa zikikosa mikakati muafaka ya kufanya usajili na   kuunda timu zinazotoa ushindani na hivyo kujikuta zikiwa washiriki tu wasiokuwa na malengo.

Usajili mbovu umekuwa ukivuruga malengo ya maendeleo ya  soka la Tanzania naklabu kwa ujumla.

Hiyo ni kwa sababu hata timu zinazopata nafasi ya kupanda daraja kucheza Ligi Kuu zimekuwa zikikosa mikakati madhubuti na kujikuta zikicheza msimu mmoja na kisha kurejea zilikotoka!

Ni vizuri  kila klabu ikafanya usajili kulingana na mahitaji yake na  kwa kuhakikisha inawashirikisha viongozi wa benchi la ufundi na  walimu wa timu, ambao ndiyo  wenye dhamana ya kubeba majukumu yote yanahusu usajili.

Tunapenda kuvikumbusha vilabu vinavyoshiriki michuano hiyo mikubwa, ambavyo mara kwa mara vimekuwa vikitangaza nia ya kubadili soka la Tanzania, viwe na mipango  mapema ya usajili na hata maandalizi ya timu endapo kweli vinataka kuondoa ufalme wa klabu kongwe za Simba na Yanga.

Tunaamini endapo maandalizi na mikakati ya kusuka vikosi bora itaanza kipindi hiki na hasa kama viongozi wataangalia walipojikwaa msimu uliopita, basi huenda ndoto za kuliona soka letu likipiga hatua zaidi, zitaweza kutimia.

Tunatambua kwamba historia imekuwa ikizibeba timu hizi, lakini mafanikio hayo siyo andiko takatifu lisilobadilika, hivyo mafanikio yanaweza kutimia kwa kila timu kufanya usajili wa uhakika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles