28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

URUSI, PHILIPPINES KUSHIRIKIANA KIJESHI

DA NANG, Vietna


SERIKALI ya Urusi imesema ipo tayari kushirikiana na Philippines katika  masuala ya kiufundi kijeshi ili kupambana na magaidi.

Taarifa hiyo ilitolewa juzi na Rais wa Urusi, Vladimir Putin wakati alipokutana na mwenzake wa Philippines, Rodrigo Duterte.

Wawili hao wameshiriki mkutano wa nchi wanachama wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kiuchumi  kwa  nchi za Asia na Pasifiki (APEC) uliomalizika jana mjini hapa.

Wakizungumza pembeni mwa  mkutano huo, Rais Putin alimkumbusha kiongozi mwenzake huyo jinsi alivyolazimika kukatisha ziara nchini mwake kutokana na matatizo ya ugaidi yaliyotokea Philippines na jinsi alivyomuomba washirikiane ili kuyatokomeza.

“Nakumbuka jinsi ulivyolazimika kukatisha ziara yako Urusi kutokana na shambulizi la ugaidi lililotokea nchini mwako na pia nakumbuka ulivyonieleza tunatakiwa kuanzisha ushirikiano  ili kuwatokomeza magaidi wote,”alisema Rais Putin katika mazungumzo hayo.

“Ningependa kukupongeza kwa kuweza kuyafanya hayo yote,”aliongeza kiongozi huyo wa Urusi.

Rais Putin alisema kupamba na magaidi ni moja kati ya changamoto kubwa baina ya nchi hizi mbili.

Alisema katika kuheshimu makubaliano hayo inabidi wapange kuongeza ushirikiano zaidi hasa katika nyanja za ufundi kijeshi na pia katika masuala ya kiuchumi.

Alisema ingawa uhusiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo mbili kwa sasa hauridhishi, katika miaka ya hivi karibuni kumekuwapo na mwamko.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles