24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Urusi, Marekani zajibizana kuhusu mapambano mapya ya silaha

WASHINGTON, MAREKANI

URUSI na Marekani zimerushiana maneno makali katika mkutano wa Umoja wa Mataifa juzi, kila mmoja akimtuhumu mwenzake kwa kutishia kuanzisha mapambano mapya ya kutengeneza silaha.

Wakati hali ikiwa hivyo kwa upande wa mataifa hayo mawili kwa upande wake  China imesisitiza  kuwa haitojihusisha kwenye makubaliano yoyote mapya ya makombora.

Mapema mwezi huu, Marekani na Urusi zilisitisha mkataba unaozuia kutengeneza makombora ya masafa mafupi – INF, uliofikiwa wakati wa enzi ya vita baridi, baada ya kila mmoja kumlaumu mwenzake kwa kukiuka makubaliano hayo.

Urusi inasema Marekani inajiandaa kwa “mashindano ya kujirundukia silaha.” Marekani kwa upande wake inasema haitaki “kupakata mikono” wakati Moscow inaendelea kujiimarisha kijeshi.

Urusi imependekeza kuitishwa kikao cha baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa baada ya Marekani kufanya jaribio la nyuklia na kufyatua kombora la masafa ya wastani mapema wiki hii.

Kombora hilo ni miongoni mwa yale ambayo yamepigwa marufuku kufanyiwa majaribio.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles