24.4 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

URUSI: MAREKANI IMETANGAZA VITA YA KIBIASHARA

MOSCOW, URUSI

WAZIRI Mkuu wa Urusi, Dmitry Medvedev amesema vikwazo vipya vilivyowekwa na Marekani dhidi ya taifa hilo ni sawa na kutangaza vita vya kibiashara.

Amesema mikakati iliyotiwa saini na  Rais Donald Trump inaonyesha udhaifu wa kiongozi huyo wa Marekani, akisema ameaibishwa na Bunge.

Sheria hiyo inalenga kuiadhibu Urusi kwa kuingilia uchaguzi wa Marekani wa 2016 pamoja na vitendo vyake dhidi ya Ukraine.

Katika kutia saini makubaliano hayo dhidi ya adui wa Marekani kupitia sheria ya vikwazo siku ya Jumatano, Trump hata hivyo alisema mkakati huo si sawa.

Sheria hiyo pia inaiwekea vikwazo Iran na Korea Kaskazini.

Iran imesema kuwa vikwazo hivyo vipya vinakiuka makubaliano ya mpango wa nyuklia na kwamba itajibu kwa njia ilio ‘sahihi na sawia’, kwa mujibu wa chombo chake cha habari cha Isna.

Haki miliki ya picha Reuters

Korea Kaskazini kwa upande wake haijatoa tamko lolote kuhusiana na hatua hiyo ya Marekani.

Medvedev pia alionya kwamba hatua mpya zinazolenga kumuondoa Rais Trump madarakani zitachukuliwa kwa kuwa si mtu aliye na utaratibu.

Moscow ambayo imekana kuingilia uchaguzi wa Marekani tayari imelipiza kisasi kwa kuwatimua maofisa 755 kutoka katika ubalozi wa Marekani nchini Urusi.

Aidha imezuia jengo moja la Marekani pamoja na ghala moja nchini Moscow.

Mataifa kadhaa ya Ulaya ikiwemo Ujerumani hayaonekani kufurahia vikwazo hivyo vipya na Rais wa Tume ya Ulaya, Jean Claude Juncker ameonya vitaathiri maslahi ya nishati ya Ulaya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles