30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Urusi kuunda intaneti yake binafsi

MOSCOW, URUSI

BUNGE la Urusi maarufu kama Duma limepitisha muswada ambao utakapokuwa sheria, utalifanya taifa hilo kubuni mfumo wake wa mtandao wa Intaneti utakaolifanya kutotegemea ule unaotumika duniani.

Muswada huo uliopitishwa kwa kura nyingi za wabunge 307 huku 68 wakiupinga, utawasilishwa katika Bunge Kuu la Urusi ili kuidhinishwa na kisha kuwasilishwa kwa Rais Vladmir Putin kutia sahihi ili kuufanya sheria kamili na kuanza kutekelezwa Novemba, mosi.

Sheria hiyo itawezesha Serikali ya Urusi kubuni miundombinu yake binafsi ya Intaneti na kuweza kusalia mtandaoni hata kukitokea dharura ya taifa lolote kujaribu kuuzima.

Mmoja wa waandishi wa muswada huo, Andrei Klishas aliliambia Shirika la Habari la Ujerumani (DW) kuwa hawana shaka Marekani ina uwezo wa kiufundi wa kuizimia Urusi huduma za intaneti wakati wowote wakipenda, hivyo wanajiandaa kiufundi kuhakikisha wanajilinda dhidi ya mashambulizi kama hayo.

Mkuu wa Kamati ya Sera na Habari, Leonid Levin alisema huduma salama za intaneti ni muhimu kwa Warusia na serikali kwa jumla.

Hadi sasa maswala ya kiufundi ya namna miundombinu hiyo itakuwa hayajakuwa bayana, lakini taasisi kuu ya mawasiliano ya Urusi – Roskomnadzor ndiyo itakuwa kituo kikuu cha kufuatilia na itasimamia intaneti hiyo kukitokea mashambulizi.

Hata hivyo, watetetzi wa haki za binadamu walisema hili linalenga kuwadhibiti wapinzani wa Serikali.

Mkurugenzi Mhandisi wa Shirika la Roscomsvoboda, Stanislav Shakirov alisema wazo hili lilianza mwaka 2012 baada ya kuanza kwa vuguvugu la mapinduzi katika mataifa ya Kiarabu na kushika kasi wakati wa mapinduzi ya Ukraine mwaka 2014.

Alisema kuanzia hapo Serikali ya Urusi iliingiwa woga kuhusu mawasiliano ya mtandao wa intaneti na sasa inajaribu kujilinda mapema iwapo kutatokea maandanano makubwa ya umma dhidi yake.

“Hii sheria ilipitishwa baada ya China kutaka kupanua huduma zake za intaneti, ila kwa sababu si rahisi kuitekeleza hapa Urusi, uwezekano uliopo ni kwamba haitaweza kutekelezwa kwa muda uliopangwa, ila itatumiwa wakati wa mapinduzi, maandamano makubwa na mengine.

Intaneti itazimwa mipakani na kila kitu kuchujwa. Wakati mwingine kitakachoweza kutekelezwa katika sheria hii ni kudhibiti yanayoendelea mitandaoni,” alisema Stanislav.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles