29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

URUSI KUONGEZA USHAWISHI ULAYA MAGHARIBI

MOSCOW, Urusi


RAIS wa Urusi, Vladimir Putin, ameelezea kwa kina kuhusu uhusiano baina ya nchi yake na Armenia zinavyoshirikiana  katika nyanja mbalimbali, zikiwamo za kisiasa na kiuchumi.

Rais Putin aliyasema hayo juzi, wakati akizungumza na Rais wa Armenia, Serzh Sargsyan, ambaye alikuwa nchini hapa kwa ziara ya kikazi.

Akizungumza na kiongozi huyo, Putin alisema kwa nchi yake, bado inaendelea kufanya kazi kwa mujibu wa makubaliano ambayo yalifikiwa wakati Rais Sargsyan alipokuja nchini hapa mapema machi, mwaka huu.

“Ningependa kutambua kwamba, timu zetu zote hufanya kazi kwa bidii juu ya utekelezaji wa mikataba yetu iliyofikiwa wakati ulipotembelea Urusi Machi mwaka huu. Mafanikio haya ni matokeo  ya ushirikiano wetu katika nyanja za mawasiliano,  kisiasa, usalama na uchumi,” alisema Rais Putin,   katika mazungumzo na rais mwenzake huyo.

Ukuaji wa uchumi ulikuwa umeanza kukua tangu mwaka jana na mwaka huu takwimu tayari zinaonesha ongezeko, jambo ambalo alidai ni kufurahisha na kwamba angependa hali hii inaendelea.

Kiongozi huyo wa Urusi alifafanua pia mbali na mafanikio hayo, pia ushirikiano wao katika masuala ya utamaduni na misaada ya kibinadamu nao unaendelea kukua kwa haraka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles