30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Upulizaji dawa mbu wa Dengue wasubiri mashine

Na TUNU NASSOR

-DAR ES SALAAM

UPULIZIAJI wa dawa za kuua mbu wanaosababisha ugonjwa wa Dengue, utaanza mara baada ya wakurugenzi kukamilisha mchakato wa ununuzi wa mashine za kupulizia.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Dk. Yudas Ndungile, alisema kwa sasa juhudi hizo ziko chini ya wakurugenzi, hivyo kazi ya ununuzi itakapokamilika kazi itaanza mara moja.

“Suala hili linasubiri wakurugenzi wa manispaa kukamilisha ununuzi wa mashine za kupulizia ndipo tutaanza mara moja,” alisema Dk. Ndungile.

Alisema kwa sasa hawezi kueleza siku rasmi ya kuanza kwa kazi hiyo kutokana na jukumu hilo kukabidhiwa kwa wakurugenzi wa manispaa.

Wiki iliyopita, akizungumza wakati wa ziara ya kukagua eneo la Jangwani, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, aliagiza kuanza kwa umwagiliaji dawa ya kuua viuadudu ikiwemo mbu pevu.

“Mvua zimeshamalizika, sasa naagiza muanze kupulizia dawa na kazi hii haitazidi siku tano, mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro na Tanga. Pia naagiza wamiliki wa baa, mahoteli, makanisa, misikiti na nyumba moja moja kuchukua hatua ya upuliziaji wa dawa hii,” alisema Ummy.

Jiji la Dar es Salaam litaanza kupuliziwa dawa ya viuadudu (Biolarvicides) ikiwamo mbu ikiwa ni sehemu ya kupambana na ugonjwa wa homa ya dengue ambayo hivi sasa ni tishio.

Kazi hiyo pia itafanyika katika mikoa ya Morogoro, Pwani na Tanga ambayo nayo imeripotiwa kukumbwa na athari za ugonjwa huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles