Imechapishwa: Sat, Aug 12th, 2017

UPINZANI WATAKA BUNGE LIVUNJWE

 

PRETORIA, AFRIKA KUSINI

CHAMA kikuu cha upinzani nchini Afrika Kusini, Democratic Alliance (DA), kimewasilisha hoja kutaka bunge la nchi hiyo livunjwe na uchaguzi uitishwe mapema, ikiwa ni siku chache baada ya hoja ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais Jacob Zuma kugonga mwamba.

Graham Charters, msemaji wa chama cha upinzani cha Democratic Alliance, amesema hoja hiyo mpya tayari imewasilishwa kwa Spika wa Bunge, atakayeamua iwapo itapelekwa mbele ya Bunge.

Zuma, mwenye umri wa miaka 75, ambaye kipindi chake cha pili na cha mwisho cha uongozi kinamalizika mwaka 2019, amenusurika mara kadhaa kuondolewa madarakani kupitia kura ya kutokuwa na imani naye, iliyoitishwa kufuatia tuhuma za rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.

Hata hivyo, chama cha ANC kimeapa kuikwamisha hoja hiyo, kama kilivyowahi kukwamisha hoja nyingine kama hizo zenye lengo la kuiangusha serikali ya chama hicho.

 

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

YOUTUBE

UPINZANI WATAKA BUNGE LIVUNJWE