25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Upepo waharibu nyumba 150

Hadija Omary, Lindi                                      

Nyumba 157 yakiwamo majengo ya serikali zimebomolewa na upepo mkali ulioambatana na mvua iliyonyesha juzi Wilaya ya Nachingwea, mkoani Lindi.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Rukia Muwango amesema mvua hiyo iliyoanza saa 10:30-11:30 jioni iliambatana naupepo mkali ambao licha ya kuharibu nyumba za kuishi katika kata za Nachingwea, Songambele na Stesheni, pia umeharibu Zahanati ya Stesheni.

Ametaja maeneo yaliyokumbwa na upepo huo katika Kata za Stesheni kuwa ni nyumba na zahanati jumla 83, Kata ya Songambele nyumba 14na kata ya Nachingwea nyumba 60 na kufanya idadi kufikia 157.

“Katika tukio hilo watu wanne wamejeruhiwa kwa kuangukiwa na kuta za nyumba zao, kisha kukimbizwa hospitali ya wilaya hiyo wakatibiwa na kuruhusiwa kurejea majumbani mwao, hakuna aliyepoteza maisha.

“Hata hivyo, bado haijafahamika hasara iliyopatikana na ofisi yake imewaagiza wataalamu kufanya upembuzi yakinifu ilikubaini thamani yake,” amesema.

Pamoja na mambo mengine, Mkuu huyo wa wilaya ametaja sababu zilizochangia uharibifu huo, ni ujenzi usiozingatia ubora ikiwamo kutokuwepo kwa linta zilizo na ubora na kutumia mbao zisizokuwa na viwango vinavyohitajika kwa ujenzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles