27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

UPASUAJI WA KIHISTORIA

  • Arekebishwa mshipa mkubwa wa moyo JKCI

NA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM

TAASISI ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), kwa mara ya kwanza imefanikiwa kufanya upasuaji wa kurekebisha mshipa mkubwa unaotoa damu kwenye moyo kwenda sehemu mbalimbali za mwili (Aortic Aneurysm Repair).

Madaktari bingwa wa JKCI, wamefanya upasuaji huo kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Saifee ya Mjini Mumbai ya nchini India.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi hiyo, Bashir Nyangassa, alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio waliyoyapata katika kambi ya matibabu iliyoanza Novemba 8, mwaka huu ikitarajiwa kukamilika leo.

“Katika kambi hii tumefanya upasuaji kwa njia ya kufungua kifua kwa watu wazima, tumepandikiza mishipa ya damu kwenye moyo kitaalamu tunaita Coronary Artery Bypass Grafting (CABG),” alisema.

Alisema kwa siku walikuwa wakiwafanyia upasuaji huo wagonjwa watatu na kwamba tayari wamefanyia wagonjwa wapatao 15.

“Ikiwa wagonjwa hawa wangeenda kutibiwa nje ya nchi Serikali ingelipa zaidi ya Sh milioni 405 kila mgonjwa angelipa zaidi ya Sh milioni 27, lakini hapa nchini kila mgonjwa amegharimu Sh milioni 15 pekee,” alisema.

Naye Daktari Bingwa wa Upasuaji Moyo wa Hospitali ya Saifee, Ali Ascar Behranwala, alisema anajivunia kufanikisha upasuaji huo.

“Tumeshirikiana vizuri na wataalamu wa hapa JKCI, nina imani kubwa kwamba utaalamu huu ambao wamejifunza kupitia kambi hii itawawezesha kuendelea kufanya upasuaji wa aina hii na hivyo kuokoa maisha ya wale watakaokuwa na matatizo ya aina hiyo,” alisema.

Alipongeza Taasisi hiyo kwa kuzidi kupiga hatua katika utoaji huduma za kibingwa za kutibu magonjwa ya moyo.

“Nimeshuhudia idadi kubwa ya wagonjwa wakipokelewa na kupatiwa matibabu dhidi ya matatizo yao na kurejea wakiwa na afya njema,” alisema.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles