23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

UN yataka ukiukwaji haki za binadamu ukomeshwe DRC

Kinshasa, DRC

MKUU wa ofisi inayoshughulikia masuala ya haki za binadamu ndani ya Umoja wa Mataifa (UN), ametoa wito kwa Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kukomesha vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu vinavyotekelezwa na majeshi ya nchi hiyo.

Katika siku ya mwisho ya ziara yake nchini DRC, Michelle Bachelet ameiambia redio ya Umoja wa Mataifa kuwa takwimu kutoka majeshi ya kulinda amani zimeonyesha kuwa majeshi na washirika wake wametekeleza zaidi ya nusu ya ukiukaji huu.

Bachelet alisema kulikuwa na mauaji ya watu 19 mwezi Novemba.

Hata hivyo, Bachelet alisema idadi ya matukio ya ukiukaji wa haki za binadamu uliotekelezwa na vikosi vya Serikali na vya waasi kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita ilishuka kiasi.

Eneo la Beni limekuwa likishuhudia matukio ya raia kuchinjwa kila uchao.

”Kama nilivyoahidi wakati wa kuapishwa kwangu, ni kwamba udhibiti wa amani katika maeneo ya Beni, Butembo katika Mkoa wa Kivu ya Kaskazini na huko Minembwe Fizi katika Kivu ya Kusini dhidi ya makundi ya uasi katika eneo lote la nchi, ni moja na itaendelea kuwa jukumu langu la kudumisha usalama katika nchi nzima,” alisema Rais Felix Tshisekedi wakati wa kampeni.

Ikiwa ni mwaka mmoja tangu Tshisekedi kuchaguliwa kuwa rais wa DRC, changamoto ya usalama eneo la Mashariki bado ni suala nyeti na limekuwa likikumbwa na msururu wa mauaji, vita pamoja na utekaji nyara wa mara kwa mara kutoka kwa waasi si tu kundi la MaiMai, lakini kubwa limekuwa hili la waasi wa ADF.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles