27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

UN yashauri chaguzi zifanyike

NEW YORK, MAREKANI

UMOJA wa Mataifa (UN) umezitaka nchi za Afrika ambazo zinatarajiwa kuwa na chaguzi wakati huu wa janga la corona, zisiahirishe chaguzi hizo bali ziwape wananchi wao haki yao hiyo ya kidemokrasia sambamba na kuchunga protokoli zote za kiafya.

Mwito huo umetolewa na Katibu Mkuu wa UN, Antonio Guterres aliyesema hayo katika ujumbe wake wa Siku ya Afrika iliyoathibiwa jana Jumatatu, Mei 25.

Alisema: “Nawaomba wanasiasa kushiriki katika mazungumzo jumuishi na endelevu ya kisiasa na kuondoa mvutano kwenye masuala ya uchaguzi na watekeleze kivitendo kanuni za kidemokrasia.”

Hivi sasa takribani nchi 20 za Afrika zinatarajiwa kuwa na uchaguzi mwaka huu, na tayari baadhi ya nchi hizo zimeonesha nia ya kusogeza mbele wakati wa uchaguzi. 

Guterres alisema, jambo hilo linaweza kuhatarisha utulivu na amani katika nchi hizo za Afrika.

Aidha katika ujumbe wake huo, Guterres alikumbushia mwito wake wa kutaka kukomeshwa mapigano ili kutoa fursa ya kupambana na janga la CovidD-19, na aliyapongeza mataifa ambayo tayari yameitikia mwito huo.

Vile vile alisema, ni masikitiko makubwa kuona kuwa maadhimisho ya siku ya Afrika yamekuja wakati wa mapambano na janga la gonjwa la corona. Hata hivyo amezipongeza nchi za Afrika kwa kuonesha uongozi wa kipekee na uratibu mzuri wa kukabiliana na Covid-19.

Katika sehemu nyingine ya ujumbe wake, Guteress amekumbusha kuwa hivi karibuni amezindua tamko la kisera la jinsi ya kuisaidia Afrika kukabiliana na corona ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha wanawake na vijana na kuweka muundo wa kipekee wa urejeshaji madeni.

AP

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles