26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

UN yaonya watoto wakimbizi kukosa elimu

BERLIN, UJERUMANI



UMOJA wa Mataifa umesema nchi zinazowapokea wakimbizi hazifanyi juhudi za kutosha kuwaingiza watoto wakimbizi katika mifumo yao ya elimu na kwamba juhudi zaidi zinahitajika  kuwajumuisha watoto hao duniani kote.

Hayo yameelezwa kwenye ripoti ya elimu iliyotolewa jana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) mjini Berlin, Ujerumani.

Ripoti hiyo; Ufuatiliaji wa Elimu Duniani mwaka 2019, imeonya kuwa watoto wengi wakimbizi bado wananyimwa elimu bora.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, nusu ya watu waliolazimika kuyakimbia makazi yao wana umri chini ya miaka 18 na mara nyingi hawana uwezo wa kujiunga na mifumo ya elimu katika nchi wanazoenda kuomba hifadhi.

Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Audrey Azoulay amesema elimu ni muhimu na kuwa watu hawataweza kusonga mbele kama elimu kwa wahamiaji na wakimbizi haipewi kipaumbele.

Kwa upande wake Manos Antoninis, mkurugenzi wa ripoti hiyo ya elimu amezionya nchi kutodhani kwamba kazi inakamilika  wahamiaji wanapoingia shule. Amesema wanakuwa wakitengwa kwa njia nyingine nyingi.

Ripoti hiyo imebainisha kuwa ukosefu wa walimu wenye ujuzi na fedha vimekuwa vikikwamisha juhudi za kuwaingiza shuleni wanafunzi wahamiaji.

Ripoti   imefafanua kuwa Ujerumani pekee inahitaji walimu wapya 42,000 kwa ajili ya kuwafundisha watoto wakimbizi waliochukuliwa kama sehemu ya sera ya Kansela Angela Merkel ya kufungua milango kwa wakimbizi iliyoanza mwaka 2015.

Chad, Ethiopia na Uganda zimepongezwa kwa kuwaandikisha wakimbizi katika shule zao, zikiwa katika kundi la nchi zenye kipato cha chini, huku Canada na Ireland zikipongezwa kwa kutekeleza sera za elimu jumuishi, katika mataifa yaliyoendelea  katika viwanda na yale yanayoendelea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles